Yanga Yawekewa Mil 300 Kuiua Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yawekewa Mil 300 Kuiua Simba-Michezoni leo

TAYARI joto la kuelekea Dabi ya Kariakoo, limeshaanza kupanda, ambapo inaelezwa kwamba, nyota wa Yanga wameahidiwa shilingi milioni 300 ili waiue Simba Jumamosi hii.

 

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa na pointi 57, ilizozivuna katika michezo 27, wakati Simba ipo kileleni ikibembea na pointi zake 61, baada ya kucheza mechi 25 tu.

 

Timu hizo Jumamosi hii zinatarajiwa kupambana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa kutoka kambini kwa Yanga huko Avic Town, Kigamboni, Dar, zinaeleza kwamba, awali wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM walitoa ahadi ya shilingi bilioni 1, kama timu hiyo itabeba ubingwa wa Ligi Kuu na FA msimu huu ambapo mchanganuo ulikuwa ni Sh milioni 300 za FA na Sh milioni 700 ligi kuu, lakini sasa wachezaji wameongezewa Sh milioni 300 endapo wataifunga Simba Jumamosi.

 

“Kusema kweli wadhamini wetu wamekuwa wakijitoa vya kutosha katika kuhakikisha tunafanya vema kwenye michuano yote iliyo mbele yetu, kwani pamoja na kuahidi kiasi cha shilingi bilioni moja kama tutatwaa ligi na FA, kuelekea kwenye dabi wameongeza tena milioni 300.

 

“Hapa kiukweli hatuna tena cha kuwalaumu GSM kama tutashindwa kuifunga Simba kisha kujiweka mahali pazuri kwenye mbio za ubingwa wa ligi na FA, maana tayari hata posho tu za mechi hiyo zimeongezeka, mwanzo ilikuwa kila tukishinda tunapewa Sh milioni 15, baadaye ikapanda hadi Sh milioni 20 ambapo kuelekea Simba wametoa Sh milioni 300, Mungu atupe nini tena,” alisema mtoa taarifa.

 

STORI NA MUSA MATEJA | GPL

The post Yanga Yawekewa Mil 300 Kuiua Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz