Yanga Waunasa Mkataba wa beki AS Vita-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Waunasa Mkataba wa beki AS Vita-Michezoni leo

DJUMA SHABANI ndilo jina ambalo linafanyiwa kazi kwa sasa na uongozi wa Yanga ili kuhakikisha wanafanikiwa kumnasa na kumsajili mchezaji huyo kwa ajili ya kurudisha makali ya kikosi hiko tayari kwa msimu ujao ambapo unaambiwa uongozi wa Yanga tayari wameshaunasa mkataba wa beki huyo.

 

Beki huyo wa kimataifa wa DR Congo anayekipiga katika Klabu ya AS Vita, amekuwa katika kiwango bora kiasi ambacho amezivutia timu nyingi Afrika ikiwepo Yanga ambayo ipo katika hatua nzuri za kumnasa.

 

Taarifa za kuaminika kutoka katika chanzo cha ndani ya Yanga, zinasema kuwa mkataba wa beki huyo upo ukingoni ukiwa umebakiza mwezi mmoja ili uweze kumalizika jambo ambalo linazidi kuipa urahisi timu hiyo kumsajili beki huyo ambaye ameonesha nia ya kutaka kujiunga na klabu hiyo msimu ujao.

 

“Yanga wameshafanya mazungumzo na uongozi wa mchezaji Djuma Shabani na wameambiwa kuwa mkataba wake utamalizika Juni 30, mwaka huu, hivyo utaona kuwa amebakiza mkataba wa mwezi mmoja pekee, kinachoendelea kwa sasa ni makubaliano ya msingi ili dili liweze kukamilika,” kilisema chanzo.

 

Kwa upande wa meneja wa mchezaji huyo, Faustino Mukandila alisema kuwa:

 

“Ni kweli tupo katika mazungumzo na Yanga ambayo kama yatakwenda vizuri basi kuna uwezekanao mkubwa wakampata mchezaji huyo, kila kitu kama kitakwenda sawa basi mtafahamu hivi karibuni.”

 

Alipotafutwa Eng.Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM juu ya kueleza usajili wa beki Djuma Shabani kuhitajika na Yanga simu yake iliita bila majibu.Yanga imedhamiria kukiimarisha kikosi chao ambapo msimu ujao wana asilimia kubwa za kushiriki michuano ya kimataifa.

STORI: MARCO MZUMBE, DAR

The post Yanga Waunasa Mkataba wa beki AS Vita appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz