Tanasha Naye Aliamsha - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Tanasha Naye Aliamsha
HAWAPOI, hawaboi! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia warembo waliowahi kuwa na uhusiano na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutengeneza matukio kila uchwao! RISASI lina jipya kutoka kwa Tanasha Donna, karibu.

 

NI BAADA YA DIVA…

Tanasha ameliamsha dude ikiwa ni wiki moja tangu, mrembo Lovness Malinzi ‘Diva The Boss’ naye aliamshe kwa kusema anampenda sana Diamond wakati kabla ilifahamika hawakuwa sawa.

 

PICHA PAAP!

 

Juzi, Tanasha alivujisha picha inayomuonesha akiwa na Diamond kwenye treni na kusindikiza na ujumbe ambao uliibua mjadala kama wote.

 

Ujumbe huo ulisomeka hivi: “Unbreakable.” Kwa tafsiri isiyo rasmi akimaanisha uhusiano usioweza kuvunjika. Shughuli ya wambeya kwenye mtandao wa Instagram ikawa ni kutaka kujua ni wapi na ni lini maana inafahamika kwa sasa Mondi yupo Sauz.“Hii ni wapi tena jamani mbona sielewi haya mapichapicha,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.

 

FULL KUISAMBAZA

Mjadala huo ulizidi kuwa mkubwa ambapo watu wengi walichukua picha hiyo na kuisambaza kwenye kurasa mbalimbali hususan zile ambazo zinadili na umbeya.

 

“Amkeni amkeni, achana na Diva ambaye yeye alimchimba kidogo Zari ambaye kwa sasa inaonekana yupo mambo yao si mchezo huko Sauz, Tanasha naye kaachia hii mbona wanatuchanganya hawa watu,” alichangia mdau mwingine mwenye ushawishi kwa umbeya mjini Instagram.

 

MONDI BIZE NA ZARI

Kabla ya Tanasha kuvujisha picha hiyo juzi, upepo wa habari ulikuwa huko Sauz ambapo Diamond ameweka kambi kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine, amekuwa akitupia picha kibao akiwa nyumbani kwa Zari.

 

Kama hiyo haitoshi, picha mpya iliyosambaa juzi imemuonesha Diamond akiwa kiwanja na Zari wakiwa ‘very close’ ile ya mtu na mtuwe kabisa.

 

Sambamba na hilo, kupitia Insta Story, Mondi ameposti video zinazomuonesha akiwafanyia shopping wanaye Tiffah na Nillan kwa kuwanunulia magari ya kifahari ya watoto.

 

TUJIKUMBUSHE

Diva naye amekuwa akikesha akimsifia Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram.Ikumbukwe kwamba, Diva na Diamond au Mondi hawakuwa wakiivana chungu kimoja kwa miaka mingi kiasi cha chuki kutamalaki kati yao.

 

Kwa kipindi chote, Diva alikuwa shabiki kindakindaki wa mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kabla ya kuhamia kwa Rajab Abdul ‘Harmonize’.Hata hivyo, kwa sasa Diva anasemekana kufika mbali zaidi kiasi cha kumchimba mzazi mwenza au baby mama wa Mondi, Zari.

 

DIVA ALIVYOJILIPUA

Baada ya kipindi kirefu, hivi karibuni Diva alianza kufunguka kwamba yeye ni shabiki namba moja wa Mondi hadi hapo atakapoingia kaburini na yupo tayari kupambana na yeyote atakayekuwa kinyume na staa huyo wa Wimbo wa Waah.Mbali na ishu za kimapenzi, Diva anasema kuwa anamkubali sana Mondi kwani anafanya kazi kwa bidii na anaona ameleta mabadiliko kwenye muziki.

 

Diva anasema pamoja na kwamba Harmonize anafanya vizuri, lakini siyo sababu ya yeye kumshindanisha na bosi wake wa zamani; yaani Diamond.Diva anaongeza kuwa, wanaomshindanisha Diamond na Harmonize wanakosea na kusema kuwa licha ya yote hayo, kizazi tulichonacho ni kizazi cha Harmonize na ni mwanamuziki anayemkubali wengine watabaki kuwa malejendi tu.

 

HUKO NYUMA…

Takriban miaka mitano iliyopita, Diva alianza kumrushia Mondi hasa akiwa hewani kwenye Radio Clouds FM kwa madai kwamba walikuwa na bifu la chinichini.

 

Vita hiyo ya maneno ya wawili hao ambao waliwahi kuimba wimbo wa pamoja wa Piga Simu, ilianza baada wawili hao kukutana kwenye Kipindi cha XXL cha Clouds FM ambapo aliyekuwa mtangazaji wa kipindi hicho, Hamis Mandi ‘B Dozen’ (kwa sasa yupo EFM) aliwauliza kama wamemaliza tofauti zao.

 

Katika majibu yake, Mondi alisema kwamba, Diva alikuwa akimsema vibaya bila sababu yoyote na hapo ndipo Diva alipodakia na kuanza kurusha maneno makali hadi walipozimiwa vipaza sauti.Katika kipindi hicho, Mondi alisikika akijiuliza ni kwa nini ‘hakumkaza’ kwani ndiyo heshima ingekuwepo.

 

Kwa upande wake, Diva alisikika akijibu kuwa, Mondi siyo ‘taipu’ yake.Hata hivyo, ilishindikana kuwatuliza wakiwa studio ndipo wakatolewa nje na baada ya hapo Diva alihamia mitandaoni na kudai kumshtaki Mondi kwa kile alichodai kwamba, jamaa huyo alimtishia kumuua.

 

Miaka kadhaa baadaye, Mondi aliibuka na kusema kwamba, chanzo cha chuki ya Diva dhidi yake ilitokana na kumnyima nafasi ya utangazaji kwenye vituo vyake vya redio na televisheni vya Wasafi Media.

 

“Diva kila siku anasumbua, ananipigia simu, anaomba kazi Wasafi TV.“Anawapigia watu wengi tu wa karibu yangu akiwemo Lilian Mwasha (mtangazaji wa Wasafi Media) na wengine.“

 

Anasema anataka kuleta kipindi chake cha usiku Wasafi TV. Mimi nimekataa, siwezi kumpokea, labda kama menejimenti watakubali, lakini mimi sitaki.

 

“Mimi nimesema sitaki aje Wasafi TV, kwa hiyo ndiyo maana hapa katikati ameongeza chuki nyingi, lakini mimi sina imani naye na sitaki kuiua Wasafi. Kwa hiyo siwezi kumpokea, kama nilivyosema sitaki, akaona afanye bifu kuwa bifu, ila mimi ninamsamehe tu bure,” anasema Mondi.
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz