SportPesa Yakabidhi Hundi ya Sh Mil 50 Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

SportPesa Yakabidhi Hundi ya Sh Mil 50 Simba-Michezoni leo

KAMPUNI ya burudani na michezo SportPesa jana imekabidhi mfano wa hundi ya Sh 50Mil kwa Simba baada ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itoke kutolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofi si za SportPesa ambao ni wadhamini wakuu zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam, Simba wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Barbara Gonzalez sambamba na benchi la ufundi.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas aliwapongeza wachezaji na viongozi wa Simba kwa hatua waliyofi kia katika michuano hiyo mikubwa Afrika.

“Nawapongeza viongozi na wachezaji wa Simba kwa kuwapa heshima kubwa Wanamsimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi kama wadhamini wenu wakuu kwa mafanikio makubwa na kupambana mpaka kufi kia hatua hii.

 

Tunachokifanya leo (jana) ni kutimiza moja ya ahadi tuliyotoa wakati tunasaini mkataba wa udhamini mwaka 2017 kuwa tutatoa bonasi ya Sh 50Mil endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itafuzu katika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Tarimba.

Kwa upande wa Simba, alizungumza Barbara na kusema: “Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji napenda kuwashukuru SportPesa kwa moyo wao na kuendelea kutupa ushirikiano na kupelekea sisi kufi ka katika hatua hii.

Naweza kusema kuwa wao ndio chachu ya maendeleo makubwa ya soka nchini ambayo sisi kama Simba tumeyaona kwa upande wetu na tutaendelea kutoa ushrikiano ili kuboresha mahusiano yetu.”

The post SportPesa Yakabidhi Hundi ya Sh Mil 50 Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz