SIMBA SC: KAMA TUNAHITAJI KUSHINDA JUMAMOSI, LAZIMA WACHEZAJI WETU WAJITOE KWA ASILIMIA 100-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

SIMBA SC: KAMA TUNAHITAJI KUSHINDA JUMAMOSI, LAZIMA WACHEZAJI WETU WAJITOE KWA ASILIMIA 100-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Simba SC umewatak wachezaji wake kujituma kwa zaidi ya asilimia 100 ili kuitoa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hayo yamesema na Afisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara kuekelea mchezo wa marudiano Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
“Kama tunahitaji kushinda jumamosi lazima wachezaji wetu wajitoe kwa asilimia 100, wanaweza wakiamua. Tunawaamini mnaweza kupindua matokeo na kuleta heshima Msimbazi. Wanasimba wanataka kufuzu, hatutaki kujitahidi, Simba sio timu ya kujitahidi, ni timu ya kufuzu,”amesema Manara katika mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa leo hoteli ya Serena, Dar es Salaam. 


Afisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo hoteli ya Serena, Dar es Salaam. 

Manara amesema mashabiki wanaiamini timu yao inaweza na wao uongozi wamejiandaa kikamilifu na mchezo wa Jumamosi wakiamini wachezaji watapokea maelekezo vizuri kutoka kwa walimu na kushinda.
Ameongeza kwamba kaulimbiu ya Simba kuelekea mchezo huo ni “Ama Zetu Ama Zao; Do or die season 2,” na kuhusu mashabiki Manara amesema Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeruhusu watu wasiozidi 10,000 kuingia uwanjani, ingawa wao wanaendelea kuomba waongezewe idadi.
Amemtaja Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, mwana SImba mzuri, Amos Makala kuwa mgeni rasmi siku hiyo.
“Tunawapa sana heshima Kaizer Chiefs, ni timu nzuri lakini tunao uwezo wa kupindua matokeo. Simba ikishinda mechi hii nchi itapata heshima, lakini pia tutakuwa tumeandika rekodi,”ameongeza.
Simba inatakiwa kushinda 5-0 ili kwenda Nusu Fainali kwa mara ya kwanza tangu 1974 baada ya kuchapwa 4-0 Jumamosi kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi wa Uwanja wa FNB, Johannesburg – jambo kocha kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa amesema linawezekana.

Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz