Simba Inawezekana Kuwafunga Kaizer Chief Kesho-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Inawezekana Kuwafunga Kaizer Chief Kesho-Michezoni leo

KAMA noma na iwe noma, Ama zetu ama zao, Do or die season 2, hiyo ni baadhi ya misemo ambayo imekuwa ikitajwa kwa wingi na mashabiki wa Simba wakiamini siyo tu meza itapinduliwa, bali hata viti na chochote kitakachotokea mbele yao wanaweza kukipindua kulekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs.

 

Kuelekea mchezo huo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amelazimika kuingia ‘chimbo’ kwa ajili ya kufukua wapi alipokosea na sasa kinachofuata ni NAHODHA msaidizi wa kikosi cha Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa licha ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyotabirika katika michezo ya hivi karibuni, bado hawajakata tamaa katika malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Yanga, juzi Jumatano waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na kufi kisha pointi 61, hivyo kuwafi kia vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ambao wamejikusanyia pointi 61 licha ya kuwa na michezo minne pungufu dhidi ya Yanga.

 

Yanga wamekuwa na mwenendo wa kusuasua ambapo katika michezo nane mfululizo iliyopita wamefanikiwa kushinda michezo mitatu pekee, wamepoteza miwili na kutoa sare kwenye tatu.Matokeo hayo yameonekana kuzidi kuwapunguza kasi Yanga katika vita ya kuwania ubingwa wa msimu huu.

 

Akizungumzia mipango yao Mwamnyeto alisema: “Ni kweli tumekuwa na mwendo wa kusuasua kwenye michezo yetu iliyopita, lakini tunaamini kuwa hiyo ni hali ya kawaida na ni suala ambalo tayari linafanyiwa kazi na benchi letu la ufundi.

“Hivyo, tunapambana kuhakikisha tunafi kia malengo yetu msimu huu ikiwemo kumaliza katika nafasi za juu, na hata kutwaa ubingwa.”Naye Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli akizungumza na Championi Ijumaa, alisema:

 

“Tunaendelea kujenga kikosi chetu, lakini pia tunaendelea kupigania malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu, changamoto ya matokeo ni kitu cha kawaida na hatuwezi kukata tamaa.”

 

UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kwa siku mbili mfululizo jana Alhamisi na leo Ijumaa wamepanga kufanya mazoezi kwa usiri na ulinzi mzito.

 

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wao wa pili wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi saa kumi kamili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Katika mchezo uliopita wa kwanza, uliochezwa Afrika Kusini, Kaizer Chiefs ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-0 yaliyofungwa na Mathoho Tower, Leonardo Castro na Samir Nurković aliyepachika mawili.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Simba, Ally Shatry alisema kuwa katika kuelekea mchezo wameongeza ulinzi katika mazoezi yao watakayofanya kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju.

 

Shatry alisema kuwa katika mazoezi hayo watakaoruhusiwa kuwepo uwanjani ni viongozi pekee, hivyo hawataruhusu shabiki wa aina yeyote.“Tupo vita kubwa hivyo ni lazima tufanye maandalizi kwa siri kubwa ili tuwashinde wapinzani wetu Chiefs katika mchezo wa marudiano tutakaoucheza Jumamosi.

 

“Hatutaruhusu shabiki yeyote na zaidi watakaoruhusiwa ni viongozi pekee, tunafahamu umuhimu mkubwa wa mchezo wetu huu.

 

Hiyo ndiyo sababu ya kutoa nafasi kwa vyombo vya habari siku ya jana (juzi) jioni kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kufanya mahojiano na wachezaji, kocha wetu Gomes (Didier) na baada ya hapo hatutaruhusu mwandishi yeyote wa habari kuingia uwanjani kwetu,” alisema kufanya mbinu zote anazoweza kuhakikisha timu yake inapindua matokeo ya 4-0 ambayo walifungwa Jumamosi iliyopita nchini Afrika Kusini.

Gomes amefunguka kuwa alilazimika kutazama kwa zaidi ya mara moja mchezo wao wa kwanza ili kuja na mikakati sahihi ya ushindi.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Gomes alisema: “Tulifanya makosa mengi katika mchezo wa kwanza hasa kwenye safu ya ulinzi, tulikuwa bora sana katika kuziba mianya ya kupenyeza mipira katikati, lakini kwa bahati mbaya hatukuwa bora kwenye mipira ya hewani na kusababisha tufungwe mabao matatu kwa njia hiyo.

 

Tulipata nafasi ya kuangalia mapungufu yetu, nami binafsi niliutazama mchezo ule mara mbili, hivyo tayari tumefanyia marekebisho matatizo yetu, na naamini kama hatutarudia makosa na tukajitoa kwa uwezo wetu wote bila shaka hakuna kinachoshindikana na tunajiamini kuwa tunayo nafasi kubwa ya kuweza kupindua matokeo.

 

“Sijui nini kitatokea Jumamosi (kesho), lakini najua tutashinda na tutatumia mbinu za tofauti kabisa kumaliza mchezo.”Morrison, Bocco, Mzamiru warudi kikosiniKatika mazoezi ya Simba, juzi Jumatano kocha huyo alionekana kuwarejesha katika kikosi cha kwanza John Bocco, Mzamiru Yassin na Bernard Morrison.

 

Kati ya nyota hao ni Bocco pekee ndiye aliyecheza mchezo wa kwanza akiingia kuchukua nafasi ya Luis Miquissone dakika ya 84, Morrison na Mzamiru hawakupata nafasi kabisa.

 

Katika mazoezi hayo Bocco, Mzamiru na Morrison walivaa jezi za mazoezi ambazo pia zilivaliwa na wachezaji wote waliocheza mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini na kupewa program maalum dhidi ya kundi la wachezaji wengine wa akiba.Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa nyota hao watatu wakawa sehemu ya mchezo wa kesho, ikiwemo kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

STORI: JOEL THOMAS NA CAREEN OSCAR

The post Simba Inawezekana Kuwafunga Kaizer Chief Kesho appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz