Rasmi, Tanzania Kupeleka Timu Nne CAF-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Rasmi, Tanzania Kupeleka Timu Nne CAF-Michezoni leo

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeweka wazi kwa kuipandanisha Tanzania kuwa kwenye nafasi ya nchi 12 zitakapoleka timu nne katika michuano ya kimataifa msimu ujao wanatoisimamia upande wa ngazi ya klabu.

 

Hiyo ni kufuatia Simba kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na kuwapiga bao Libya.

 

CAF imeipandisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 12 ambazo zinapeleka timu nne msimu ujao wa 2021/22 ambapo mbili zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na zingine Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Kwa mujibu renki za CAF, Tanzania imepanda hadi nafasi ya 12 ikiishusha Libya iliyokuwa katika nafasi hiyo ambayo imeteremshwa kwa nafasi tatu ikiwa pointi 13.5.Kitendo cha Simba kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, kimeifanya Tanzania kukusanya pointi 27.5.

 

Spoti Xtra limezungumza na Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Salum Madadi ambaye amefafanua juu ya timu ambazo zitakuwa na nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

 

“Nafasi ya kupeleka timu nne namna ilivyo ni kwamba, mbili zitatoka kwenye ligi kuu kwa maana ya mshindi wa kwanza na wa pili, na zingine mbili katika Kombe la FA kwa zile ambazo zimecheza fainali.

 

Lakini ikitokea bingwa wa ligi kuu ameingia fainali ya Kombe la FA, basi atakwenda kuiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa halafu mshindi wa pili wa FA atakwenda Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya hapo mshindi wa pili wa ligi atakwenda Ligi ya Mabingwa na mshindi wa tatu atacheza Shirikisho,” alisema Madadi.

 

KAULI YA AZAM

Mkuu wa Idara ya Habari ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka za Kazi’, amezungumzia suala hilo akisema kwa upande wao walishajiandaa mapema kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

 

“Binafsi Azam, haikushangazwa juu ya suala hilo kupata nafasi nne kwa kuwa tayari tulishajiandaa mapema kushiriki michuano ya kimataifa kupitia ubingwa wa ligi kuu au Kombe la Shirikisho, hivyo hata kama hizo nafasi zisingekuwepo bado sisi malengo yangekuwa hivyo ndiyo maana tunaendelea kupambania ubingwa.

 

YANGA WANASEMAJE?

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Hassan Bumbuli, amebainisha kwamba: “Kitu ambacho huenda hakifahamiki ni kwamba Yanga ipo kwenye malengo makubwa ya kucheza michuano ya kimataifa, lakini siyo kwa sababu ya hizo nafasi za upendeleo.“Kitu pekee ambacho tunachokiamini ni kushinda ubingwa wa ligi kuu au Kombe la FA ili tuweze kupata nafasi ya uhakika, lakini siyo hiyo ambayo imekuwa ikitajwa.”

Stori: Ibrahim Mussa, Dar

The post Rasmi, Tanzania Kupeleka Timu Nne CAF appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz