Nabi Hataki Sare Yanga, ni Ushindi Tu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Hataki Sare Yanga, ni Ushindi Tu-Michezoni leo

 

KATIKA kuhakikisha Yanga wanapata ushindi katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Namungo FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo kwa lengo la kubakia kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Yanga ambao kwa sasa wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 57 nyuma ya vinara Simba wenye pointi 61, kesho Jumamosi watacheza dhidi ya Namungo FC katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

 

Kocha huyo amesema kuwa anachokikata kutoka kwa wachezaji katika mchezo huo ni kuweza kupata ushindi kwa kuwa ndiyo lengo kuu katika mechi zao zote zilizobakia kwa sasa licha kutambua ugumu uliopo dhidi ya timu hiyo.

 

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya benchi la timu hiyo ni kuwa tayari Nabi ameshatoa majukumu kwa wachezaji kuelekea katika mchezo huo na matokeo ambayo anayahitaji ili kuweza kujiweka katika wakati mzuri wa kupigania ubingwa.

 

“Kocha amewaambia wachezaji na amekuwa akiwasisitiza kwamba ushindi katika mchezo wa Jumamosi ni kitu muhimu kutokana na presha ambayo upande wetu kwa sasa lakini ugumu wa timu ambayo tunacheza nayo.

 

“Kitu kikubwa amewataka wapambane, wajue ukubwa na thamani yao hasa katika mechi hizi ambazo zimebakia na hata katika mazoezi ambayo yamekuwa yakifanyika huku Mtwara hilo ndiyo jambo amekuwa akilipigia kelele wakati wote,” alisema mtoa taarifa.

The post Nabi Hataki Sare Yanga, ni Ushindi Tu appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz