Nabi Awaondoa Mastaa Watatu Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Awaondoa Mastaa Watatu Yanga-Michezoni leo

KIKOSI cha Yanga leo kitajitupa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma bila ya nyota wake watatu tegemeo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.Yanga ilikuwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 58, itajitupa kwenye mchezo huo ikiwa na hasira ya kutoka kupata suluhu dhidi ya Namungo FC.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli, alisema kuwa katika kuelekea mchezo timu hiyo, kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi atawakosa wachezaji wake watatu muhimu.

 

Bumbuli aliwataja wachezaji hao ni Mukoko Tonombe, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao wote wana majeraha tofauti yatakayowasababishia kuukosa mchezo huo.

 

Alisema kuwa timu hiyo jana alfajiri ilisafiri kwa ndege kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya JKT Tanzania ambao muhimu kwao kupata matokeo mazuri ya ushindi.

“Kwa mujibu wa kocha Nabi katika kuelekea mchezo wetu wa ligi dhidi ya JKT atawakosa wachezaji wake nyota watatu waliokuwepo katika kikosi cha kwanza katika michezo iliyopita ya ligi.

 

“Wachezaji hao ni Tonombe yeye alipata maumivu ya bega, tupo naye kwenye msafara ulioondoka leo (jana) alfajiri kuelekea Dodoma kucheza na JKT katika mchezo wa ligi tutakaoucheza kesho (leo).

 

“Tumekuja naye baada ya kupata nafuu atakawepo katika mchezo ujao wa FA dhidi ya Mwadui, Ninja na Carlinhos wenyewe bado wanaendelea na matibabu ambao hawatakuwepo sehemu ya kikosi kwa kuanzia mchezo na JKT na huo wa FA ambao hawapo katika msafara wetu,” alisema Bumbuli.

 

Katika hatua nyingine wachezaji na viongozi wa Yanga jana walitembelea Bungeni, Dodoma jana wakati Bunge likiendelea na kikao cha 30, jijini hapo.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA,Dar

The post Nabi Awaondoa Mastaa Watatu Yanga appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz