Mondi Kuwakutanisha Zari, Tanasha na Mobeto - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mondi Kuwakutanisha Zari, Tanasha na Mobeto

SIMBA ameamua! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusoma taarifa hii inayomhusu supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na ma-baby mama wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Hamisa Mobeto na Tanasha Donna.

 

Habari za ndani kabisa zinaeleza kwamba, jamaa huyo amepanga kuwakutanisha wote kwa mara ya kwanza kwenye sehemu moja; yawezekana hotelini au nyumbani.

 

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Diamond au Mondi, ma-baby mama hao watatu watakutana Dar au hata nje ya Dar kutegemeana na mahali mwamba huyo atakapopanga kukutana nao.Kabla ya kurejea Dar, wikiendi iliyopita Mobeto na Tanasha walikuwa Zanzibar ambako Mondi naye alikuwa ameweka kambi, lakini ambaye alikosekana ni Zari pekee.Hata hivyo, kuna madai kwamba, naye alitarajiwa kutua visiwani Zanzibar.

 

Moja ya vyanzo vya ndani vililithibitishia Gazeti la IJUMAA kwamba, ni kweli Mobeto na Tanasha walikuwa Zanzibar.

 

Kwa upande wake, Tanasha alithibitisha uwepo wake visiwani Zanzibar baada ya kuposti picha na video zikimuonesha akiwa kwenye mazingira hayo.

 

Kuna madai kwamba, pamoja na kwenda Zanzibar kukamilisha projekti yake mpya ya muziki, lakini pia Tanasha alikwenda kumaliza tofauti zake na Mondi ambaye kwa siku za usoni amekuwa akimtuhumu kumtelekeza mtoto wao, Naseeb Junior kwa kutotoa pesa za matunzo.Mondi alitua Zanzibar siku chache baada ya kurejea Bongo akitokea nchini Afrika Kusini alikoweka kambi kwa ajili ya kuandaa albam yake mpya, lakini pia alitumia wasaa huo kujiachia na wanawe, Tiffah Dangote na Prince Nillan aliozaa na Zari.

 

Kama zoezi hilo likifanikiwa, basi itakuwa ni mara ya kwanza kwa wamama hao watatu kukutana sehemu moja wakiwa na Mondi hivyo litakuwa ni tukio la kihistoria.Itakuwa shuguli pevu kumuona laivu Mobeto na Tanasha wakicheka pamoja na hasimu yao, Zari.Zari amekuwa akiwatuhumu Mobeto na Tanasha kumuibia Mondi wake.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA juu ya uwezekano wa tukio hilo, dada wa Mondi, Esma Khan alisema hakuna cha ajabu na kwamba kila kitu kinawezekana.“Unajua wale wana damu yetu kwa hiyo sioni kama kuna linaloshindikana kukutana na kukaa pamoja kama familia,” alisema Esma
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz