Mchepuko Aua Mme wa Mtu Kisa Wivu wa Mapenzi - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mchepuko Aua Mme wa Mtu Kisa Wivu wa Mapenzi

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Bw. Alfred Nombo (28) kwa kosa la kuumuwa Bw. Erasto Nchimbi (28) mkazi wa Kijiji cha Sara wilayani Mbinga kwa kumchoma na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa amewaambia waandishi wa habari jana Alhamisi, Mei 20, 2021 kuwa tukio hilo limetokea Mei 19, mwaka huu, majira ya saa 4 asubuhi.

 

Alisema kuwa Nombo alikuwa na wivu wa kimapenzi kwa mke wa Nchimbi na kuamua kumuua kwa kumchoma na kisu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

 

Kamanda Maigwa alisema kuwa Bw. Nombo alinogewa na mapenzi ya mke wa marehemu Nchimbi kiasi cha kupelekea kuvunja ndoa yao na wivu uliomfanya afanye maamuzi ya kumuuwa mwenye mke ili apate nafasi ya kuwa huru na mke wa Bw. Nchimbi.

 

Aidha, Kamanda Maigwa ametoa wito kwa watu wenye uhasama kupeleka matatizo yao katika vyombo vya usuluhishi badala ya kujichukulia maamuzi ambayo yanagharimu maisha ya watu na kuishia jela.

 

Wakati huo huo Kamanda Maigwa ameelezea uchunguzi wa tukio la mwananfunzi aliyejinyonga kwa kutumia kamba ya manila Sophia Mbano (19) mwananfunzi wa kidato cha tano katika sekondari wa wasichana ya St. Agnes Peramiho chanzo kimebainika kuwa ni msongo wa Mawazo ambao umepelekea kifo chake.

 Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz