Lamine Moro Afunguka Kurudishwa Dar-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Lamine Moro Afunguka Kurudishwa Dar-Michezoni leo

MAPEMA jana Jumamosi, zilisambaa taarifa za Nahodha wa Yanga, Lamine Moro kuondolewa kambini na kurudishwa Dar wakati timu hiyo ikiwa Ruangwa mkoani Lindi ilipoenda kupambana na Namungo FC.

 

Sababu za kutimuliwa kwake, zilielezwa na Yanga kwamba ni utovu wa nidhamu hali iliyomfanya kocha mkuu wa kikosi hicho, Nasreddine Nabi kumuondoa.

 

Yanga ambayo jana ilipambana na Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi, iliondoka Dar Jumatano iliyopita tayari kwa mchezo huo.

 

Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa, amebainisha kwamba: “Lamine hakuwa sehemu ya kikosi kwa sababu ni majeruhi, lakini alisafiri na timu ili kuangalia program za mwalimu kwa wenzake.“Lakini kwa bahati mbaya akatofautiana na kocha ambaye anasimamia misingi ya nidhamu, akaamuru arudishwe Dar.

 

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Lamine Moro aliandika: “Habari zenu, tafadhali ikiwa umesikia kitu juu ya mtu jaribu kujua kinachoendelea kabla ya kusema chochote juu ya mtu huyo. Asanteni.”

 

Mbali na posti yake hiyo, Spoti Xtra lilimtafuta Lamine kumsikia anasemaje juu ya tuhuma hizo za utovu wa nidhamu, alijibu kwa ufupi: “Kwa sasa sijisikii vizuri kuzungumza, nitafute wakati mwingine.”

STORI: JOEL THOMAS NA LUNYAMADZO MLYUKA, DAR

The post Lamine Moro Afunguka Kurudishwa Dar appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz