Kessy Aandaliwa Mkataba Mnono Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kessy Aandaliwa Mkataba Mnono Yanga-Michezoni leo

BAADA ya kuondoka Yanga misimu miwili iliyopita, beki wa pembeni, Hassan Kessy, anatajwa kuwa mbioni kurejea kwenye kikosi hicho kwa mara nyingine tena.

 

Taarifa za ndani kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa Kessy anatazamwa kuja kuwa mbadala wa Shomari Kibwana ambaye amekuwa akicheza kwenye nafasi ya beki wa kulia msimu huu.Mtoa taarifa huyo aliliambia Championi Ijumaa kuwa: “Uongozi upo kwenye mpango wa kumpa mkataba mpya Hassan Kessy kwa ajili ya kuja kucheza kama namba mbili akisaidiana na Kibwana.

 

“Uongozi unamtaka Kessy kwa ajili ya mashindano ya kimataifa msimu ujao, kilichofanya wamtazame yeye ni kwa sababu ana uzoefu wa mechi za kimataifa akiichezea Nkana The Red Devils ya Zambia pamoja na Taifa Stars.”

 

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro ili kujua ukweli wa taarifa hizo alisema: “Kiukweli nikisema ndiyo au hapana vyote itakuwa ni uongo, ukweli ni kwamba focus yetu ipo kwenye nusu fainali ya Azam Sports Federation na kuwania ubingwa wa ligi.

 

Msikilize Kessy mwenyewe: “Kusema ukweli mkataba wangu na Mtibwa Sugar unamalizika mwishoni mwa msimu na kwa sasa nipo huru kuongea na timu yoyote, habari za Yanga ni mpya kwangu lakini ikitokea wananihitaji nitakwenda kucheza kwa sababu ni kati ya timu zilizonipa heshima.”

 

Kessy aliwahi kucheza Yanga kwa misimu miwili kuanzia 2016-18, akijiunga na timu hiyo akitokea Simba, kisha 2018 akatimkia Nkana alikocheza kwa misimu miwili, kabla ya kurejea nchini na kusaini kandarasi ya miezi sita kukipiga na Mtibwa Sugar.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

The post Kessy Aandaliwa Mkataba Mnono Yanga appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz