Kajala: Sitaki Kumsikia Harmonize - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kajala: Sitaki Kumsikia Harmonize
KWA mara ya kwanza tangu apate msala mzito, staa mkubwa wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Mama Paula, ametema nyongo akisema kwamba hataki kusikia swali kuhusu aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’.

 

Hivi karibuni, Kajala amekumbana na misukosuko kutokana na ishu ya binti yake kudai kutongozwa na Harmonize au Harmo.

 

Mbali na hilo, pia kuna kuvuja na kusambaa kwa video chafu ya Harmo iliyodaiwa kutoka kwa Paula ikimhusisha pia mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny ’ ambao wote waliishia kutiwa mbaroni na kuhojiwa Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

 

Baada ya hayo yote, Gazeti la Ijumaa limefanya jitihada za kumpata Kajala kwenye mahojiano maalum (exclusive interview) ambaye ameweka wazi kuwa hata yeye ni binadamu mwenye nyama na mifupa.

 

Kajala anasema kuwa, watu wengi wanamfikiria kwamba yeye kama binadamu hana maumivu kama mama wanavyomsema mtoto wake na wanavyomzungumzia yeye mwenyewe, lakini wangejua siri ya mtungi wangenyamaza.Katika mahojiano hayo ya ana, staa huyo wa filamu na Tamthiliya za Kibongo anafunguka mengi juu ya sakata hilo;IJUMAA: Mambo vipi Kajala, pole na misukosuko…

 

KAJALA: Asante, hii ndiyo dunia, tunaona na kushuhudia mambo mbalimbali.IJUMAA: Ndiyo ukubwa huo, je, unaendeleaje sasa hivi?

 

KAJALA: Niko poa sasa hivi, lakini siyo kihivyo ila Mungu wetu, hajawahi kutuacha hata siku moja.

 

IJUMAA: Naona sasa hivi hata kwenye mitandao unaingia kwa mbali sana tofauti na zamani, je, kwa nini.

 

KAJALA: Hakuna raha ya mitandaoni hata kidogo, kwanza ni kujiumiza maana ukikatiza tu, mara wamekuandika hivi, wamemuandika mtoto wangu vile, kwa kweli inaumiza mno. Ninachojua watu wamesahau mimi ni binadamu, nina nyama na mifupa kama wao, wangejaribu kufikiria maana wengine ni wamama kabisa kama mimi.

 

IJUMAA: Vipi kuhusu ishu ya Polisi, maana tuliona kwenye mitandao ya kijamii, mkiwa mnaingia kwenye gari?

 

KAJALA: Mimi hayo sipendi kuyaongelea kabisa kwa sasa kwa sababu sipendi kumnufaisha mtu yeyote.

 

IJUMAA: Lakini hivi sasa unaendelea na mambo yako kama kawaida?

 

KAJALA: Maisha lazima yaendelee, hakuna kilichobadilika kwenye maisha yangu hata siku moja. Cha muhimu nimejifunza mambo mengi kwenye maisha yangu kwa kipindi hiki hivyo nitaendelea kujifunza kila siku.

 

IJUMAA: Ulishawahi kuzungumza na Harmonize baada ya tukio lililotokea?

 

KAJALA: Sitaki kusikia mambo hayo kwa sasa, ningeachwa kwanza.IJUMAA: Pia naona kama umepoa sana kwenye sanaa, kulikoni?

 

KAJALA: Ni kweli, lakini siyo kwamba nimeacha. Ni vitu viliingiliana, lakini nitaendelea tu.

 

IJUMAA: Vipi kuhusu yule PCK; mwanaume ambaye anasisitiza kuwa alikuwa na wewe Dubai na ndiye aliyekupia kila kitu?

 

KAJALA: Mtu mwerevu hawezi kuchukua anachoongea yule, kwanza ananikera sana kwa kweli na hata waandishi waangalie watu wa kuwahoji, nachukizwa mno na huyo mtu anayejiita sijui nani maana hata jina siwezi kulitaja.

 

Nasema kama ana ushaidi wa kile anachokisema au hata wa chumba atoe, hebu aachane na mimi, siyo wa kumpa kiki, aende hukohuko kwa aliowazoea na sina la zaidi la kusema (akiomba kukatisha mahojiano).

 

IJUMAA: Basi nashukuru sana Kajala kwa ushirikiano wako…

 

KAJALA: Asante, nisamehe kwa leo, bado sipo okey, lakini siku nyingine nitawapa mahojiano mazuri zaidi.
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz