Global Yaichapa VIA Veteran Bao 1-0-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Global Yaichapa VIA Veteran Bao 1-0-Michezoni leo

WABABE wa soka, Global FC, juzi Ijumaa walifanya ubabe wao mbele ya VIA Veteran baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Tegeta, Dar.

 

Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia zaidi, ilishuhudiwa Global FC ikicheza kandanda safi lililowafanya mashabiki waliojazana uwanjani hapo kutoa sifa kemkem, huku kipindi cha kwanza kikiisha kwa 0-0.

 

Kipindi cha pili wakati mchezo ukiendelea huku VIA Veteran wakifanya mashambulizi bila mpangilio, beki wa kushoto wa Global FC, Omary Mdose akaunasa mpira na kuituliza timu, kisha akaanzisha shambulizi ambalo lilitua mguuni mwa Thomas Mselem aliyetoa pasi kwa Francis Rweyemamu ‘Chichi’ ambaye bila ajizi, akampa asisti mfungaji David Kanyenye aliyeutumbukiza kimiani mpira na kuadika bao hilo pekee la ushindi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Global FC, Philip Nkini, amesema: “Mchezo ulikuwa mzuri japo uwanja ulitukaba, lakini tuliweza kupata matokeo mazuri kutokana na mazoezi ya kutosha tuliyokuwa tukiyafanya.

 

“Endapo uwanja ungekuwa mzuri, nina uhakika tungepata ushindi wa mabao si chini ya matano kutokana na uimara wa timu yetu unaoambatana na maandalizi mazuri kila siku.

 

Naye Nahodha wa VIA Veteran, Ally Mororo, amesema: “Tunamshukuru Mungu tulianza na kumaliza salama. Mchezo ulikuwa mzuri, tulipata nafasi nyingi lakini hatukuweza kuzitumia vizuri, wenzetu wakazitumia hadi kupata matokeo mazuri.“Uwanja haukuwa rafiki sana kwetu, hivyo tunajipanga mechi ijayo tusawazishe makosa yetu.”

The post Global Yaichapa VIA Veteran Bao 1-0 appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz