Carlinhos Anaitaka Simba Tu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Carlinhos Anaitaka Simba Tu-Michezoni leo

Carlinhos

PAMOJA na kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Angola, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo maarufu Carlinhos, kuumia na kutolewa uwanjani juzi Ijumaa kwenye mechi dhidi ya Prisons, lakini imebainika kwamba mwamba huyo anawataka kwa hamu Simba.

 

Carlinhos alitolewa uwanjani akibebwa kwenye machela dakika ya 64 baada ya kuumia katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambapo Yanga ilishinda 1-0 na kutinga robo fainali.

Jumamosi hii ambapo Yanga itakuwa mgeni wa Simba, Carlinhos anatarajiwa kuwepo uwanjani ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Taarifa kutoka Yanga zinasema kwamba, Carlinhos hakupata majeraha makubwa ya kumfanya kutocheza mechi yao na Simba, hivyo mwenyewe amesema yuko fiti na anaitaka namba yake kuivaa Simba.

 

“Carlinhos hakupata majeraha makubwa kama wengi walivyodhani baada ya kushindwa kuendelea na mechi yetu dhidi ya Prisons, mimi nimekuwa naye jana baada ya mechi tu na mwenyewe amesema anahamu kubwa ya kuhusika katika mchezo ujao dhidi ya Simba kwani yupo fiti,” kilisema chanzo kutoka Yanga.

 

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Wachezaji wakifika Dar tunatarajia kuwafanyia vipimo, baada ya hapo ninaamini tutakuwa na taarifa juu yao ila kwa sasa ninachojua ni kwamba wote wanaendelea salama.”

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA, SPOTI XTRA

The post Carlinhos Anaitaka Simba Tu appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz