Breaking: Zidane Anasepa Tena Madrid-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Breaking: Zidane Anasepa Tena Madrid-Michezoni leo

TAARIFA zilizoripotiwa na vy9ombo vya habari vya Hispania zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amethibitisha kuwa ataondoka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu hata kama atachukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania LaLiga.

 

Madrid ambao ambao jana wamekipiga na Granada na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu kwa kuifunga bao 4-1 wakiwa ugenini, kwa sasa wapo katika nafasi ya pili ya msimamo wa LaLiga wakiwa na pointi 78 nyuma ya Atletico Madrid ambao wana pointi 80 na michezo miwili imesalia kumalizika kwa ligi hiyo.

Zidane (48) akiwa Madrid ameshinda mataji mawili ya Laliga na mataji matatu ya UEFA Champions League kwa misimu minne ambayo ameitmikia klabu hiyo lakini ameamua kuondoka klabuni hapo baada ya mechi yao ya mwisho ya ligi dhidi ya Villarreal itakayopigwa May 23, Santiago Bernabeu.

 

Zidane atakuwa chagua la kwanza la Juventus na Timu ya taifa ya Ufaransa iwapo watafanya mabadiliko ya kocha baada ya Fainali za Euros zinazotarajiwa kuanza Juni 11.

Rais wa Madrid, Florentino Perez yupo katika wakati mgumu kusaka mbadala wa Zidane ambapo inaelezwa anataka kumpandisha Kocha Raul kuchukua mikoba ya Zizzou ama atamchukua tena kocha Max Allegri.

 

Zidane amesema anahisi hayuko kwenye moyo wa Perez and hata kama atachukua taji la LaLiga kwa mara ya tatu, rekodi ambayo atakuwa ameiweka ya kurudisha kombe la laliga kwa misimu miwili mfululizo.

 

Zidane ameingia kwenye headline baada ya kutofautiana na mchezaji wake, beki kisiki Marcelo raia wa Brazil baada ya kumuacha katika kikosi chake kilichocheza na Granada huku ikielezwa kuwa wawili hao hawana mahusiano mazuri klabuni hapo kwa sasa.

Marcelo atamaliza mkataba wake baada msihoni mwa msimu huu. Marcelo anasema Zidane amekuwa mtu wa kukosoa sana katika mazoezi wakati akizungumza na timu yake kuhusu ushindi wa mechi zake, lakini pia alizungumza mbele ya meneja wa timu kuhusu kuamua kumuacha Marcelo na kumchukua kinda wa miaka 19, Miguel Gutierrez kuanza.

 

Inaelezwa kuwa, kinda huyo ambaye ameuibua Zidane wiki chache zilizopita ndiyo anaweza kuwa nguzo pekee ya kumbakisha Zizzou Madrid.

The post Breaking: Zidane Anasepa Tena Madrid appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz