Zuma atakiwa kuchagua adhabu kwa kosa la kudharau mahakama - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Zuma atakiwa kuchagua adhabu kwa kosa la kudharau mahakama

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa mpaka Jumatano kupendekeza adhabu ambayo mahakama kuu ya nchi hiyo inapaswa kutoa ikiwa atapatikana na hatia ya dharau.
Adhabu hiyo inahusiana na kupuuza kwake wito wa kufika mbele ya tume ya uchunguzi inayoongozwa na Jaji Ray Zondo kujibu tuhuma za ufisadi - ambazo amekuwa akikana.

Mwezi Januari, mahakama ya katiba ya nchi hiyo ilimwamuru afike mbele ya tume hiyo, lakini akapuuza agizo hilo.Mwezi uliopita, tume hiyo iliitaka mahakama imhukumu rais huyo wa zamani kwa miaka miwili, ili kuonesha uzito wa vitendo vya Bw Zuma.

Mahakama hata hivyo ilizuia uamuzi katika kesi hiyo.Bwana Zuma wakati huo alisema haogopi kwenda gerezani ikiwa mahakama zitaamua hivyo - akielezea kwamba hakujitokeza mbele ya tume kwa sababu alikuwa amepoteza uaminifu kwenye mifumo ya haki.

Wakati huo huo mahakama ya rufaa Jumanne ilitetea uamuzi wa awali kwa serikali kupata pesa ambazo ilikuwa imezitumia kwa ada ya kisheria ya rais wa zamani.

Ilisema ufadhili wa serikali katika kesi hiyo ya ufisadi ulikuwa "haramu, kinyume cha katiba na ni batili".Inakadiriwa kuwa serikali ililipa kati ya dola milioni moja na milioni 2.2 kama gharama katika kesi hiyo.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz