Yanga Yatoa Tamko kwa TFF Adhabu ya Mwakalebela-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga Yatoa Tamko kwa TFF Adhabu ya Mwakalebela-Michezoni leo

KLABU ya Yanga imepinga adhabu iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya kumfungia Makamu Mwenyekiti wake, Fredrick Mwakalebela, kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi pamoja na faini la jumla ya Sh. milioni saba kwa makosa ya kimaadili.

 

 

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Haji Mfikirwa, amesema wao kama viongozi wa Yanga hawajaridhishwa kabisa na adhabu hiyo, hivyo wanajiandaa kupinga hukumu hiyo kwa njia zilizowekwa kwa kikatiba na kistaarabu.

 

 

Hata hivyo, alisema kuwa tamko rasmi la klabu hiyo litatolewa na Mwenyekiti, Dk. Mshindo Msolla kutokana na jambo lenyewe linamhusu makamu mwenyekiti. “Msimamo rasmi wa klabu utatolewa na Mwenyekiti kwa sababu jambo linamhusu makamu mwenyekiti.

 

 

Kwa ukubwa huo ni busara likaongelewa na mwenyekiti, lakini sisi kama klabu kwa haraka haraka hatujaridhishwa na uamuzi huo,” alisema Kaimu Katibu huyo na kuongeza.

The post Yanga Yatoa Tamko kwa TFF Adhabu ya Mwakalebela appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment