Yanga Yaingilia Usajili wa Beki wa Kibabage-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga Yaingilia Usajili wa Beki wa Kibabage-Michezoni leo

BAADA ya Simba kuwa katika mipango ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Tanzania, Nickson Kibabage, hatimaye Klabu ya Yanga nayo imeingilia kati dili hilo kwa ajili ya kutaka kumsajili beki huyo ambaye ameonekana kuwa tishio.

 

Hivi karibuni uongozi wa Simba ulikutana na mchezaji huyo kwa mazungumzo ya kutaka kumsajili alipokuwa nchini katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, lakini kwa sasa inaripotiwa Yanga pia imeingilia kati dili hilo ikijaribu kumshawishi ili akubali kujiunga na timu hiyo.

 

Kibabage kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Youssoufia FC ya nchini Morroco, akitokea kwa mkopo katika Klabu ya Difaa Hassan El Jadid ya nchini humo.

 

Chanzo cha uhakika kutoka Yanga kililiambia Championi Jumatano, kuwa timu hiyo ipo katika mipango ya kuboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao haswa katika eneo la beki wa kushoto jambo ambalo limewafanya kuanza kuingia sokoni mapema huku Kibabage akiwa mmoja kati ya mapendekezo yao.

 

“Ni kweli Yanga tupo katika mpango wa kuendelea kukisuka kikosi chetu kwa ajili ya mipango yetu ya baadaye na moja kati ya sehemu ambazo zinatakiwa kufanyia maboresho ni pamoja na eneo letu la ulinzi wa kushoto.

 

“Ndiyo maana umeona kuna tetesi nyingi zinatuhusisha na wachezaji wa maeneo hayo, kuhusiana na Kibabage ni moja kati ya wachezaji wazuri katika eneo la ulinzi wa kushoto, ni mchezaji ambaye tumekuwa tukimfikiria kuwa moja kati ya sehemu ya wachezaji wetu,tutaona itakuwaje mwisho wa msimu huu,” kilisema chanzo hiko.

 

Alipotafutwa beki Nickson Kibabage juu ya kuhitajika ndani ya Yanga aligoma kabisa kusema chochote juu ya taarifa hizo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

 

 

The post Yanga Yaingilia Usajili wa Beki wa Kibabage appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.