WEST BROM YAICHAPA CHELSEA 5-2 PALE PALE DARAJANI-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

WEST BROM YAICHAPA CHELSEA 5-2 PALE PALE DARAJANI-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

TIMU ya West Bromwich Albion leo imeichapa Chelsea 5-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, hicho kikiwa kipigo cha kwanza kwa kocha Thomas Tuchel.
Katika mchezo huo ambao Chelsea ilimaliza pungufu kufuatia kutolewa kwa Thiago Silva kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, mabao ya West Brom yamefungwa na Matheus Pereira dakika ya 45+2 na 45+4,  Callum Robinson dakika ya 63 na 90 na ushei na Mbaye Diagne dakika ya 68, wakati ya The Blues yamefungwa na Christian Pulisic dakika ya 27 na Mason Mount dakika ya 71


No comments:

Post a Comment