UEFA Yaipeleka Chelsea Hispania-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

UEFA Yaipeleka Chelsea Hispania-Michezoni leo

MICHEZO ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Chelsea na Porto sasa itapigwa katika Jiji la Sevilla nchini Hispania.

 

Mechi hizo mbili zitapigwa katika Uwanja Ramon Sanchez- Pizjuan tofauti na awali michezo hiyo ingepigwa London, England na Lisbon, Ureno.

 

Hii ni kutokana na ndege kutoka England kwenda Ureno zimepigwa stop ndiyo maana mchezo huo umepelekwa Hispania kutokana na janga la virusi vya corona.

 

Ureno awali iliondolewa kwenye orodha kwa ndege zake kuingia England, ila sasa mambo yamebadili na timu hizo zimelazimika kupangiwa sehemu nyingine.

 

Michezo hiyo ambayo itapigwa huko, Sevilla wa kwanza Chelsea atakuwa ugenini na wa pili atakuwa nyumbani.

 

Taarifa ya UEFA ilieleza: “Kama Shirikisho la Soka Ulaya, mechi za Chelsea na Porto hatua ya robo fainali kwa sasa zimehamishiwa katika Uwanja wa Ramon Sanchez- Pizjuan pale Sevilla na zitachezwa kati ya Aprili 7, na 13.

 

“UEFA inawashukuru Chelsea na Porto kwa kutoa ushirikiano na sapoti katika hilo kupitia vyama vyao vya soka pamoja na Hispania.”

The post UEFA Yaipeleka Chelsea Hispania appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment