Simba Wakutana Kujadili Ofa ya Manula-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba Wakutana Kujadili Ofa ya Manula-Michezoni leo

BAADA ya mabosi wa timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kuzidi kuwa ‘siriaz’ na ishu ya kuipata saini ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula, leo uongozi wa Simba unatarajiwa kukaa chini kujadili ofa ya mchezaji huyo pamoja na ofa za wachezaji wengine.

 

Manula amekuwa kwenye kiwango msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa amecheza jumla ya mechi tano kwenye hatua za makundi na kukusanya clean sheet tatu na ameokota nyavuni mabao mawili.

 

Timu yake pia imetinga hatua ya robo fainali jambo ambalo limezifanya timu nyingi Afrika ikiwa ni pamoja na Al Merrikh nayo kuipigia hesabu saini ya Manula ambaye ni mzawa.

 

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Simba zimeliambia Championi Jumamosi kuwa kesho (leo) Bodi ya Wakurugenzi ya Simba itakaa kujadili ofa za wachezaji wao huku kipaumbele ikiwa ni Manula.

 

“Mamelodi Sundowns pamoja na timu nyingine zimeonekana kuwa hazitanii kwa kuleta ofa ambapo tayari bodi ya Simba inatarajiwa kukaa kesho (leo) kujadili suala la wachezaji wao ambao wanahitajika na timu nyingine.

 

Kutokana na ofa ilivyo inaonekana kwamba mambo yatakwenda vizuri hivyo baada ya kikao itajulikana hatma ya Manula ndani ya Simba pamoja na wachezaji wengine,” alisema mtoa taarifa huyo aliyeomba hifadhi ya jina.

 

Mamelodi Sundowns inahitaji mbadala wa Denis Onyango raia wa Uganda ambaye alisema kuwa ana mpango wa kustaafu huku dau ambalo wamemuwekea Manula linatajwa kuwa shilingi milioni 500 ili kupata saini yake.

 

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, hivi karibuni alisema kuwa ikiwa watapokea ofa kutoka timu inayohitaji mchezaji wa timu hiyo hawataweza kukataa ikiwa itawafaa na mchezaji mwenyewe akakubali kuondoka.

STORI NA MUSA MATEJA, Dar es Salaam

The post Simba Wakutana Kujadili Ofa ya Manula appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.