SAMATTA AFUNGA BAO PEKEE FENERBAHCE YASHINDA 1-0 KATIKA LIGI KUU YA UTURUKI-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

SAMATTA AFUNGA BAO PEKEE FENERBAHCE YASHINDA 1-0 KATIKA LIGI KUU YA UTURUKI-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

BAO pekee la Mbwana Ally Samatta leo limeipa 
Fenerbahçe ushindi wa 1-0 dhidi ya Denizlispor katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki Uwanja wa Ülker Fenerbahçe Şükrü Saracoğlu Spor Complex Jijini İstanbul.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania mwenye umri wa miaka 28, alifunga bao hilo dakika ya 64 akimalizia pasi ya beki Mturuki, Caner Erkin. 
Kwa ushindi huo, Fenerbahçe inafikisha pointi 62 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Beşiktaş inayoongoza na mechi moja mkononi, wakati Denizlispor inayobaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 30 inaendelea kushika mkia.


No comments:

Post a Comment