Saido Apewa Jukumu Zito Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Saido Apewa Jukumu Zito Yanga-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’, amepewa jukumu zito na kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi kwa kuhakikisha anapambana na wachezaji wenzake kuisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu.

Mwambusi leo Jumamosi ataiongoza Yanga katika mchezo wake wa kwanza akiwa kaimu kocha mkuu dhidi ya KMC katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa huku ukiwa ni mchezo wake wa kwanza baada kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Cedric Kaze.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi limezipata kutoka ndani ya timu hiyo, kiungo huyo ni mmoja kati ya wachezaji waliopewa majukumu makubwa na kocha huyo kwa kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa msimu licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa Simba.

 

“Mikakati imekuwa mingi sana kwa kuwa timu inataka kupata ubingwa na ndiyo limekuwa lengo kubwa kwa sasa maana wapo wachezaji waliotakiwa wabadilike na wapo waliopewa majukumu kutokana na uzoefu wao.

 

“Sasa mtu Ntibazonkiza kocha ametaka kwanza kujitoa na kuendelea kuwa kiongozi ndani na nje ya uwanja kutokana na uzoefu wake lakini kuhakikisha Yanga inapata matokeo zaidi katika kila mchezo ambao itacheza,” alisema mtoa taarifa.

 

Saido aliyejiunga na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu, mpaka sasa ameifungia timu hiyo mabao matatu katika michezo mitatu aliyocheza kwenye ligi kuu.

STORI: IBRAHIM MUSSA,Dar es Salaam

The post Saido Apewa Jukumu Zito Yanga appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz