Okwi: Simba Itacheza Fainali CAF-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Okwi: Simba Itacheza Fainali CAF-Michezoni leo

STAA wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema wala haitashangaza kuona timu hiyo ikitinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na kulichukua kombe.

 

 

 

Okwi ambaye alitamba na Simba, huku pia akipita Yanga, ameitaja Simba kuwa ni moja kati ya timu bora Afrika kwa sasa na imecheza kwa kiwango cha juu sana msimu huu na wanastahili kupata mafanikio makubwa.

 

 

Kauli ya Okwi imekuja wakati huu ambao Simba imetinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kinara wa Kundi A mbele ya Al Ahly.“Simba wanamshangaza kila mpenda soka kwa sasa Afrika, kitendo cha kumaliza kundi wakiwa vinara mbele ya timu kama Al Ahly na AS Vita siyo jambo dogo, hiyo inaonesha kuwa wapo imara na ni timu bora kwa sasa Afrika.

 

 

“Haitashangaza kuona wanacheza fainali na hata kuchukua kombe lenyewe, wanastahili kupata mafanikio makubwa msimu huu kutokana na jinsi kikosi chao kilivyo bora,” alisema Okwi na kuongeza.

 

 

“Tanzania kwangu naona ni kama nyumbani kwa sababu nimeishi na watu wake vizuri, halafu ninaipenda sana hasa klabu yangu ya Simba ambayo nilicheza kwa muda mrefu.

 

 

“Ninaipenda kwa kuwa ndiyo imebadilisha maisha yangu katika sehemu kubwa, lakini pia imenipa heshima hadi hapa ambapo nimefi ka, hivyo najivunia kuipenda Simba.

 

 

Kwa sasa Okwi anakipiga kwenye timu ya Al Ittihad Alexandria inayoshiriki Ligi Kuu Misri na juzi Ijumaa alikwenda jijini Cairo kuishuhudia Simba ikicheza na Al Ahly kwenye mchezo ambao Simba walifungwa 1-0.

 

ISSA LIPONDA NA IBRAHIM MUSSA

 

The post Okwi: Simba Itacheza Fainali CAF appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz