Mwambusi Aifumua Yanga, Ataja Sehemu Zenye Matatizo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwambusi Aifumua Yanga, Ataja Sehemu Zenye Matatizo-Michezoni leo

KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, Jumamosi iliyopita aliiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kukabidhiwa mikoba, akaambulia sare ya 1-1 dhidi ya KMC.

 

Sasa baada ya mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Mwambusi amesema atafanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa Jumamosi ijayo uwanjani hapo.

 

Mwambusi ambaye anaiongoza Yanga baada ya Kocha Cedric Kaze kutimuliwa Machi 7, mwaka huu, amezitaja sehemu ambazo zimeonekana kuwa na matatizo sugu kwamba ni safu ya ulinzi na ushambuliaji.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwambusi alisema: “Baada ya kupata sare na KMC, kikosi kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Biashara United.

“Tunafahamu kwamba tunapaswa kufanya vizuri katika mchezo huo ili tupate ushindi na kurejesha hali ya kujiamini na ushindani katika kuelekea kufikia malengo ya kuwa mabingwa.

 

“Kuelekea mchezo dhidi ya Biashara, tutaendelea kuona mabadiliko katika nafasi kadhaa ndani ya uwanja, ikiwemo kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi kama ambavyo tuliona dhidi ya KMC ambapo Abdallah Shaibu ‘Ninja’ alianza.

 

“Tunafanya hivi ili kuona tunapata uwiano mzuri wa matumizi ya wachezaji wetu na kupunguza makosa yetu, ili kuhakikisha tunamaliza kiu ya mashabiki wetu ya kukosa ushindi kwa muda mrefu.”

The post Mwambusi Aifumua Yanga, Ataja Sehemu Zenye Matatizo appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz