Mondi, Zari Waharibiana Swaumu - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mondi, Zari Waharibiana Swaumu

  



WAMEHARIBIANA swaumu! Ndiyo kauli iliyopigiwa mstari na baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislam baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutua Afrika Kusini na kuandaliwa futari na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

Hatua hiyo imetafsiriwa na baadhi ya viongozi hao wa Dini ya Kiislam kuwa wamekiuka maadili ya dini hiyo hususan katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hasa ikizingatiwa Zari siyo mke halali wa Diamond au Mondi, bali ni mzazi mwenzake tu.

 

Hayo yamejiri baada ya Mondi kukwea pipa kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo Zari anaishi na watoto wake wawili Latifah Nasibu ‘Tiffah dangote’ na Nillan ‘Prince Nillan’.

 

Aidha, Zari na Mondi ambao wote ni waumini wa Dini ya Kiislam, wameonekana wakifurahia maisha ya pamoja na watoto wao tangu alipotua nchini humo mapema wiki hii.

 

Mmoja wa waumini wa Dini ya Kiislam aliyejitambulisha kwa jina la Aziz Hashim alifafanua kuwa; “Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, hairuhusiwi wapenzi kukutana, haijalishi hata kama mlishaachana, mkikutana tu mnakuwa tayari mmeshaharibu swaumu, kwa hiyo jambo alilolifanya Mondi kwenda Sauzi kwa Zari kisha Zari naye kumpokea tayari wameshaharibu swaumu yao.”

 

Kauli hiyo iliungwa mkono na Sheikh Ahmed Kandauma ambaye alisema kwa mujibu wa taratibu za Quran, wawili hao wamekiuka maandiko ya kitabu hicho kitakatifu na kuvunja kanuni za moja ya nguzo tano za Uislamu ambayo mojawapo ni kufunga.

 

MONDI AMEKWENDA KUFANYA NINI?

Hivi karibuni kabla hajaondoka nchini, Mondi aliweka wazi kuwa, anaelekea nchini Afrika Kusini kufanya maandalizi ya album yake ambayo anatarajia kuiachia mwaka huu kama Mungu akipenda.

 

“Nasafiri kwenda South (Sauzi) kwa ajili ya kwenda kurekodi album yangu ambayo kama Mungu akipenda Inshaallah, basi tunaweza kuiachia mwaka huu, hivyo nitakaa huko kwa muda wa mwezi mzima,” alisema Mondi.

 

Gazeti la IJUMAA lilifanikiwa kuzungumza na mtu wa karibu wa familia hiyo ambapo alisema kuwa, ni kweli Mondi amesafiri kwenda nchini humo, lakini kwa kipindi cha muda f’lani atakaa kwa mzazi mwenzake huyo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wake.

 

“Mondi lazima akae kidogo na watoto wake kwa sababu wewe mwenyewe si unajua kwamba ni muda mrefu umepita tangu akutane nao? Halafu kuhusu huyo King Bae wa Zari, Mondi wala hana shida naye, wao wamebaki kama wazazi tu,” anasema mtu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

 

SHANGWE KAMA LOTE

Aliyesema wazazi hawaachani wala hakukosea kwa sababu baada ya staa huyo kutua mjengoni kwa mjasiriamali Zari, shangwe zilikuwa kama zote, huku watoto wao, Tiffah na Nillan wakionekana kuwa karibu zaidi na baba yao.

 

“Mmmh! Jamani mbona kama Zari anajibebisha sana kwa Mondi? Yaani anavyokaa naye karibu ni kama vile anatamani warudiane ila ndiyo haiwezekani tena,” aliandika shabiki mmoja mitandaoni.

 

TUJIKUMBUSHE

Zari na Mondi wamewahi kuwa kwenye mahaba mazito na kufikia hatua hadi ya kuzaa watoto wao wawili, lakini baadaye walitengana huku chanzo cha kuachana kwao kikitajwa kuwa ni usaliti wa kimapenzi baada ya Mondi kudaiwa kumsaliti Zari kwa kutembea na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto ambaye naye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Abdul Nasibu ‘Dyllan’.

 STORI: MEMORISE RICHARD, DAR




Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz