Lulu, Majizzo Baada Ya Ndoa Kimya Kimya.. Sherehe Harusi Yanukia - EDUSPORTSTZ

Latest

Lulu, Majizzo Baada Ya Ndoa Kimya Kimya.. Sherehe Harusi Yanukia
UNAAMBIWA baada ya msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mmiliki wa kituo cha EFM na TVE, Francis Ciza ‘Majizzo’ kufunga ndoa ya kimyakimya, inadaiwa kuwa, hivi karibuni wawili hao wanatarajia kuangusha bonge la sherehe.

 

Akizungumza na RISASI, mtu wa karibu na familia hiyo kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa wawili hao kwa sasa wana mpango wa kufanya sherehe kubwa itakayoacha watu midomo wazi.“

 

Lulu na Majizzo kwa sasa wapo katika mipango ya kufanya sherehe kubwa ya harusi yao, tena kwa nilivyosikia itakuwa ni bonge moja la sherehe, hivyo watu watarajie vitu vizuri tu,” alisema mtu huyo.

 

NI LINI NA WAPI?

Hata hivyo, RISASI lilivyoendelea kumchimba mtu huyo ili aeleze kiundani zaidi ishu hiyo iko vipi, alisema kuwa bado hajajua itafanyikia Dar sehemu gani lakini anachokifahamu ni kwamba itafanyika baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

 

“Kiukweli bado sijajua itafanyikia Dar sehemu gani ila ninachojua mimi ni kwamba itafanyika baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kumalizika,” alisema mtu huyo.Jitihada za kuwapata wawili hao ili kuweza kuzungumzia sherehe hiyo hazikuzaa matunda kufuatia simu zao kutopatikana.

 

Akizungumza kupitia TVE hivi karibuni, Majizzo alisema waliamua kufunga ndoa hiyo bila kufanya sherehe kubwa kwa ajili ya kuwatia moyo vijana kwamba kuoa si lazima uwe na uwezo mkubwa wa kifedha.Alisema mara baada ya kufunga ndoa kanisani, kila mmoja alishika njia yake na kwenda kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

 

Alipoulizwa kama wazazi, ndugu, jamaa na marafiki walipokeaje uamuzi wao huo, Majizzo alisema waliwaelewesha na wakaelewa.

 

TUJIKUMBUSHE

Februari 16, mwaka huu Lulu na Majizzo walifunga ndoa ya siri katika Kanisa la Katoliki la Mt. Gasper lililopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Ndoa yao ilikuwa gumzo sana kutokana na usiri walioamua kuufanya ambapo siku hiyo, waandishi mbali na vyombo vya Majizzo vya habari, walizuiwa kuchukua matukio kanisani hapo huku ulinzi ukiwa mkali.
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.