Kocha Ibenge Atamba Kushinda Kesho dhidi Ya Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Ibenge Atamba Kushinda Kesho dhidi Ya Simba-Michezoni leo

KOCHA wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa hawako tayari kujiweka kwenye presha kubwa katika mchezo kesho dhidi ya Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni na aina yoyote ya matokeo yatakayopatikana watayapokea.

 

Ameyasema hayo leo Aprili 2 kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa kundi A utakaochezwa kesho.

“Siku zote tumekuwa tukifurahia kucheza na ni furaha kubwa zaidi kucheza na timu kama Simba ambayo ni miongoni mwa timu bora na nzuri Afrika.

 

Tulicheza mechi ya kwanza kule DR Congo na tukashindwa kufanya kama tulivyotarajia tukapoteza mchezo hivyo tumekuja hapa tukiamini tukicheza kama tulivyopanga tutapata matokeo tunayoyahitaji.

 

Tunafahamu tunahitajika kupata ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu lakini mwisho wa siku huu ni mpira wa miguu na tuko tayari kupokea matokeo yoyote iwe tutashinda, kutoka sare au kufungwa,” alisema Ibenge.

 

Kipa wa timu hiyo, Nathan Mabrouk alisema wanafahamu ugumu wa kucheza na Simba lakini wako tayari kukabiliana nao.

 

“Wachezaji wote tuko tayari na akili yetu tumeilekeza kwenye mchezo huu ambao tunahitajika kupata ushindi,” alisema Mabrouk.

 

Vita yenye pointi nne, inahitaji matokeo ya ushindi tu katika mechi ya kesho dhidi ya Simba ili iweke hai matumaini yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

The post Kocha Ibenge Atamba Kushinda Kesho dhidi Ya Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.