Chama, Kagere Kupambana na Mwadui Leo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Chama, Kagere Kupambana na Mwadui Leo-Michezoni leo

CLATOUS Chama, mwamba wa Lusaka ambaye ametupia mabao 7 pamoja na Meddie Kagere mwenye mabao 11, idadi ya mabao ambayo wamefunga ni sawa na yale yaliyofungwa na wapinzani wao Mwadui FC.

Jumla ya mabao ya nyota hao wawili ni 18 wakiwa wamecheza mechi 21, huku safu ya ushambuliaji ya Mwadui FC ikiwa imefunga mabao 18 baada ya kucheza mechi 25.

 

Leo Jumapili kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, timu hizo zitapambana ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili baada ya mzunguko wa kwanza, Simba kushinda 5-0 Uwanja wa Uhuru, Dar.

 

Utakuwa ni mchezo wa ushindani ndani ya dakika 90 kwa kuwa Mwadui FC inapambana kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa nafasi ya 18 na pointi 16, huku Simba ikipambana kutetea taji la ligi, ina pointi 49 ipo nafasi ya tatu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Maandalizi ya kikosi chetu kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui yamekamilika kwa asilimia kubwa, hatuwadharau wapinzani wetu kutokana na matokeo yao yaliyopita, lakini pia tumekuja hapa kwa lengo moja kubwa nalo ni kuchukua pointi zote tatu.

 

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, alisema: “Tumeweka wazi mara kwa mara kuwa malengo yetu ni kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kuhakikisha tunashinda michezo yote iliyo mbele yetu, hivyo tumesafiri kuja Shinyanga kwa ajili ya kutekeleza hilo.”

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA JOEL THOMAS

The post Chama, Kagere Kupambana na Mwadui Leo appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz