Yanga Yataja Mambo Matatu Aliyowafanyia Magufuli-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yataja Mambo Matatu Aliyowafanyia Magufuli-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

WAKATI taifa likiwa kwenye majonzi mazito na maombolezo ya siku 21 ya kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Klabu ya Yanga imetaja mambo matatu mazuri aliyowafanyia katika utawala wake.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Rais Magufuli afariki dunia kabla ya jana Rais Mama Samia Hassan Suluhu kuapishwa Ikulu ya Dar es Salaam.Rais Magufuli alifariki Jumatano jioni kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaimu Katibu Mkuu, CPA Haji Mfikirwa pamoja na kutoa salam za Rambirambi alisema chini ya uongozi wa Rais Magufuli nchi imepiga hatua kwenye sekta ya michezo.

 

Mfikirwa alisema kuwa kwa upande wao Yanga Rais Magufuli ameifanyia mengi makubwa klabu hiyo na kati ya hayo yapo matatu ambayo hawatayasahau ambayo ni;“Moja, alitaka kuiona michezo iwe ya kisasa ili tuweze kushindana na klabu kubwa barani Afrika kupitia hotuba zake alizokuwa akizitoa Rais Magufuli ambayo ilitutaka kuingia kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu na sisi kama Yanga ndiyo tunaenda nayo.

 

“Pili, alitusaidia kuziba mianya ya dhuluma kwa klabu, awali mapato ya klabu na serikali yaliyopotea sana, lakini alituletea mfumo wa N-Cards ambao klabu sasa hivi zinapata mapato yake halali viwanjani.“

 

Tatu, alikuwa rais wa bahati kwa Yanga, kwani katika mechi zetu alizohudhuria mara zote tulishinda. Nakumbuka alikuja kwenye Dabi ya Kariakoo na tukashinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Morison (Bernard), hivyo kwetu alikuwa rais wa bahati sana,” alisema Mfikirwa na kuongeza kuwa;“Kutokana na kuwa na mafanikio kwetu, na dhamira yetu msimu huu ni kutwaa ubingwa, iwapo tutafanikiwa kuuchukua, basi ubingwa tutautoa kama zawadi kwake katika kumkumbuka Rais Magufuli.

 

“Na mwisho, kwa niaba ya uongozi niombe bendera zote za klabu yetu kuanzia hapa makao makuu na matawi yote nchini, bendera zote zipepee nusu mlingoti kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha kipenzi chetu, Rais Magufuli kwa muda uliotangazwa na Serikali,” alisema Mfikirwa.

The post Yanga Yataja Mambo Matatu Aliyowafanyia Magufuli appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz