Wasudan Wampa Gomes Siri za Al-Merrikh-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wasudan Wampa Gomes Siri za Al-Merrikh-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Simba, raia wa Ufaransa, Didier Gomes Da Rosa, ameshtuka na kuwataka wachezaji wake wajipange haswa, hiyo ni baada ya kupenyezewa taarifa kutoka kwa marafiki zake wa Sudan kuwa wenyeji wao, Al-Merrikh wameupania mchezo huo.

 

Mechi hiyo ya raundi ya tatu ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kupigwa saa 10:00 jioni huko Sudan huku Simba ikiwa inaongoza kundi lao kwa kuwa na alama sita na wenyeji hawana yoyote, timu zote zimecheza mechi mbilimbili.

 

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumamosi, kwamba, pamoja na Simba kupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, bado kocha wao Gomes amepata taarifa za siri alizopenyezewa na marafiki zake wa Sudan, wakimtaka ajipange kwa kila idara kutokana na wapinzani wake kupania sana mchezo huo.

“Kabla ya kuanza safari ya kuelekea Sudan, kocha alikaa na wachezaji na kuwasisitiza namna alivyopewa siri za wapinzani wake na marafiki waishio mjini Khartoum, ambapo walimsisitiza sana kujiandaa kwa kila hali kwani mashabiki na uongozi wa Al-Merrikh umecharuka kwa kuhitaji ushindi, hivyo na yeye amewapa siri hiyo wachezaji kwa kuwataka kwenda kucheza mpira wa kasi na nguvu ili kupata mabao ya mapema.

 

“Mbali na hivyo hata leo asubuhi (jana) nimewasiliana na kocha na ameendelea kuwasisitiza sana wachezaji waachane na dhana ya kuwaona wapinzani wetu kama wanyonge kwa kuwa walipoteza mechi mbili, badala yake muda wote wafikirie namna ya kupata pointi tatu ambazo zitatuwezesha kwenye mechi za marudiano bila presha ya aina yoyote,” kilisema chanzo hicho.

 

Akizungumzia mchezo huo kabla ya kusepa, Gomes alisema: “Wachezaji wangu wote wako fiti tayari kwa kuisaidia Simba kupata matokeo.”

STORI: MUSA MATEJA, Dar es Salaam

The post Wasudan Wampa Gomes Siri za Al-Merrikh appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz