Utafiti: Wanaume Wanaathirika Zaidi na Covid 19 Kuliko Wanawake - EDUSPORTSTZ

Latest

Utafiti: Wanaume Wanaathirika Zaidi na Covid 19 Kuliko Wanawake

 


Umoja wa Mataifa umesema Virusi vya Corona vinasababisha vifo kwa Wanaume wengi zaidi Barani Afrika kuliko Wanawake ambao wao wanaandamwa na kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi


Utafiti uliofanyika kwenye Nchi 28 za Afrika, ikiwemo #Guinea, #Mauritius na #Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya Wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na Wanaume


Takwimu zinaonesha asilimia 41 ya Wanawake Barani Afrika ndiyo wamekumbwa na Janga la Corona lakini idadi hiyo inatofautiana miongoni mwa Mataifa


Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema kwa Wanawake janga la COVID19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzaziNo comments:

Post a Comment