Tonombe, Kaizer Chiefs Ishu Ipo Hivi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Tonombe, Kaizer Chiefs Ishu Ipo Hivi-Michezoni leo

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa haujapokea ofa yoyote kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini juu ya kiungo wao mkabaji Mkongomani Mukoko Tonombe kuhitajika huko.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu zizagae tetesi za kiungo huyo aliyejiunga na Yanga katika msimu huu akitokea AS Vita ya Kinshasa, Congo kuwaniwa na Chiefs.

 

Tetesi hizo zilianza kuzagaa mara baada ya gazeti hili kuandika taarifa ya Skauti Mkuu wa Klabu ya Kaizer Chiefs, Walter Steenbok kutua nchini na kwenda kutembelea ofisi za klabu hiyo na kikubwa kujionea jinsi inavyojiendesha baada ya kupata taarifa za Tonombe na Tuisila Kisinda kujiunga na klabu hiyo msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya Chiefs na Yanga kuhusiana na Tonombe.Bumbuli alisema kuwa kilichopo hivi sasa ni mahusiano mazuri waliyoyajenga hivi karibuni kati ya Yanga na Chiefs katika kupata maendeleo ya soka nchini.

Aliongeza kuwa kwa upande wao Yanga hawana tatizo, hivyo wapo tayari kupokea ofa ya mchezaji yeyote kutoka klabu yoyote itakayomhitaji Tonombe na msataa wao wengine.

 

“Hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya Yanga na Chiefs, zaidi nizikaribishe klabu ambazo zitawahitaji wachezaji wetu.

“Yanga ni kati ya timu ambazo zimefanya usajili mzuri wa wachezaji wengi walio bora, hilo lipo wazi kabisa na hiyo ndiyo sababu ya sisi kuongoza ligi,” alisema Bumbuli.

The post Tonombe, Kaizer Chiefs Ishu Ipo Hivi appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz