Simba Yamalizana na Jembe la AS Vita-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Yamalizana na Jembe la AS Vita-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

ASILIMIA 90, Simba imemalizana rasmi na beki wa kulia wa AS Vita, Mkongomani Djuma Shaban na msimu ujao atavaa jezi zenye rangi ya nyeupe na nyekundu.

 

Beki huyo ni kati wachezaji walioipa ugumu Simba kupenya kwenye ng’ombe ya Vita huku akisababisha mashambulizi kadhaa kwenye goli la wapinzani wake hao.

Mkongomani huyo alionyesha kiwango hicho katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Kinshansa, DR Congo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 kwa njia ya penalti lililofungwa na Chris Mugalu.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Simba imemalizana rasmi na beki huyo na msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi hicho.Mtoa taarifa huyo kilichobakia kwa beki huyo ni kusaini mkataba pekee baada ya klabu yake kutoa baraka ya kuja kujiunga na Simba.

 

Aliongeza kuwa beki huyo ambaye dau la usajili limefichwa alipendekezwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Mfaransa Didier Gomes katika kukiimarisha kikosi chake katika msimu ujao.

 

“Katika kuiimarisha safu yetu ya ulinzi, benchi la ufundi limependekeza kumsajili beki wa kulia wa AS Vita, Djuma atakayekuja kusaidiana na Kapombe (Shomari).

“Viongozi tayari wamelikamilisha hilo kwa kuwafuata mabosi wa Vita kwa ajili ya kumalizana na kwa asilimia 90 limefanikiwa hilo baada ya kufikia muafaka mzuri wa kukubali kumuachia ili msimu ajiunge na timu.“

 

Kocha Gomes ndiye aliyependekeza usajili wake baada ya kuvutiwa naye katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tuliocheza DR Congo,” alisema mtoa taarifa huyo.Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Anorld Kashembe kuzungumzia hilo alisema: “Muda wa usajili bado na hivi sasa timu ipo kwenye michuano ya mikubwa ya Afrika, hivyo ni ngumu kuzungumzia masuala ya usajili.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Simba Yamalizana na Jembe la AS Vita appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz