SIMBA SC WAONDOKA NA AISHI MANULA AKIWA FITI KABISA KUWAFUATA EL MERREIKH NCHINI SUDAN-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

SIMBA SC WAONDOKA NA AISHI MANULA AKIWA FITI KABISA KUWAFUATA EL MERREIKH NCHINI SUDAN-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha wachezaji 25 cha Simba SC kimeondoka Dar es Salaam jioni ya leo kwenda Khartoum, Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa tatu wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, El Merreikh Jumamosi.
Mechi hiyo itakayochezwa Saa 4:00 usiku Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman na kuonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya ZBC2 inayopatikana kwenye kisimbusi cha Azam TV inafuatia Simba kushinda mechi zake mbili za awali nyumbani na ugenini.
Ilianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita mjini Kinshasa kabla ya kwenda kuwachapa na mabingwa watetezi, Al Ahly 1-0 Dar es Salaam.
Kipa namba moja wa timu, Aishi Salum Manula aliyeumia juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanznaia Bara, Simba SC ikiichapa JKT Tanzania 3-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam amepona na amesafiri pia.
Aishi aliumia baada ya kugongana na Danny Lyanga wa JKT Tanzania hadi kupoteza fahamu na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na Beno Kakolanya.
Kikosi cha Simba kilichoondoka ni makipa; Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim.
Mabeki; David kameta, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Peter Maduhwa, Mohammed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Kennedy Juma.
Viungo; Thadeo Lwanga, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Muzamil Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Miraj Athumani, Clatous Chama na Francis Kahata.
Washambuliaji; Meddie Kagere, John Bocco na Kope Mugalu.


Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz