Neymar Ajinasia Kidege Emilia Wa Argentina-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Neymar Ajinasia Kidege Emilia Wa Argentina-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

NYOTA anayesakata kabumbu katika klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya nchini Ufaransa, Neymar da Silva Santos Júnior ‘Neymar’ (28), amepata hifadhi mpya ya penzi lake kwa mwanamuziki maarufu raia wa Argentina, Emilia Mernes.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la nchini Uingereza, wawili hao walianza kubadilishana arafa za kimahaba baada ya Emilia kuhudhuria hafla ya kufunga mwaka 2020, iliyoandaliwa na Neymar jijini Rio de Janeiro nchini Brazil.

 

Dhifa hiyo ya siku tatu iliyopewa jina ‘Neymarpalooza’, ilihudhuriwa na watu 500 wakiwemo wanamitindo Kiki Passo, Michelle Nevius na Jessica Bartlett kutoka Amerika.

 

Vile vile, makahaba Camila Remedy na Fernanda Brum kutoka Brazil walikuwepo.Siku ya mwisho Neymar alionekana akisakata densi na Emilia (24), huku wakiimba kwa pamoja kibao cha hivi punde cha mwanamuziki huyo wenye mashairi haya: “Siendi tena msituni kuwinda wakati kuna mbalamwezi. Waambie vipusa wanaokufuata kwamba mimi ni chaguo lako.

”Akihojiwa na The Sun Januari mwaka huu, Lizardo Ponce ambaye ni rafiki wa karibu wa Emilia, alikiri kwamba Neymar alimtembelea kidege huyo nchini Argentina majuma baada ya pati hiyo.“Emilia amekuwa akimsifia sana Neymar jinsi alivyomridhisha chumbani, alivyo mkarimu na pia mcheshi.

 

Hata hivyo, taarifa za wadaku zinasema kuwa hali ilivyo, kilele cha urafiki wao ni ndoa.Tuwape muda; yaliyopo kati yao yatajitokeza,” alieleza Lizardo na kuongeza kwamba dalili zote zinaashiria wawili hao wanakula bata na haitakuwa ajabu wakivishana pete za uchumba karibuni.Baada ya mahojiano hayo, Neymar alipakia kwenye Instagram picha yake na Emilia.

 

Naye kidosho huyo akajibu kwa picha nyingine akitia ‘emoji’ za furaha na kuandika: “Nakupenda kwa moyo wangu wote na mimi huamini katika miujiza ya mwanzo kuwa ni bora kwa kila jambo jipya.”Tangu Neymar atemane na mwigizaji.

aji raia wa Brazil, Bruna Marquezine, staa huyo wa zamani wa Barcelona ametoka kimapenzi na vidosho wa kila sampuli, akiwemo mwanamitindo raia wa Amerika, Natalia Barulich.

 

Sasa amejinasia kidege Emilia wa ArgentinaHata hivyo, walitengana mwanzoni mwa Desemba 2020 baada ya nahodha huyo wa timu ya taifa ya Brazil kuanza kummendea kimapenzi mwanamitindo na mwanahabari wa Uhispania, Melodie Penalver.

 

Awali, gazeti la Proto Thema nchini Ugiriki lilisema kwamba Neymar alikuwa radhi kuliwania upya tunda la Bruna baada ya Melodie kuanza kumfungulia mzinga mwigizaji Cristian Jerez aliyewahi kushirikiana naye kuendesha kipindi cha ‘Temptation Island’ kwenye mojawapo ya runinga za Uhispania.Neymar amekuwa singo tangu atengane rasmi na Bruna aliyemburudisha kimapenzi kwa miaka sita.

 

Hadi kufichuka kwa uhusiano wake na Emilia, Neymar aliwahi pia kuchovya kwenye mizinga ya warembo Liza Brito, Danna Paola, Mari Tavares, Larissa de Macedo Machado almaarufu Anitta na Ellen Santana aliyetawazwa mshindi wa Miss BumBum nchini Brazil mnamo 2018.

 

Penzi la Neymar limewahi pia kuwaniwa na vipusa Giovanna Lancelotti, Sabine Jemeljanova, Selena Gomez, Soraja Vucelic, Chloe Grace Moretz, Noa Saez, Izabel Goulart na Alsessandra Ambrosio.

 

Neymar ana mtoto mmoja wa kiume Davi Lucca da Silva Santos aliyezaliwa na mrembo raia wa Brazil, Carolina Dantas, 27, mnamo Agosti 24, 2011.Mmoja wa mashabiki wa Emilia kwenye Instagram aliandika: “Nashawishika kuiamini safari hii ya mapenzi. Tamanio langu sasa ni kuona Neymar na Emilia wakila yamini ya ndoa.

Makala: MWANDISHI WETU NA MITANDAO

The post Neymar Ajinasia Kidege Emilia Wa Argentina appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz