Nandy, Mafiga matatu yatakuponza, Unachanja Mbio Kuelekea Porini - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nandy, Mafiga matatu yatakuponza, Unachanja Mbio Kuelekea Porini


 Imeandikwa na Mshana JR

Kila mtu ana kipawa, talanta na kipaji chake , lakini kati ya hivyo vitatu kimoja ndio hujitokeza zaidi na kwa baadhi viwili ndio huonekana zaidi


Talanta na kipawa hivi viko kiroho na kiimani zaidi huku kipaji kikiwa kiko kimwili na kidunia zaidi. Kwenye hii dunia kuna falme kuu mbili , ufalme wa Nuru na ufalme wa giza...ufalme wa nuru uko kiimani zaidi kwa maana ya Kimungu na ufalme wa giza uko kidunia zaidi kwa maana ya shetani ...hizi ni falme mbili zisizochangamana


Nandy binti mwenye kipaji cha uimbaji kupitia nyimbo zilizomtambulisha za kidunia alianza na kufanya vema sana kwenye hii kaliba, lakini sasa anapotea..anachanja mbuga kuelekea porini...Pengine kwakuwa jasiri muongoza njia hayupo tena..


Pressure ya kubaki kileleni, mashindano ya vipaji vipya na ugumu wa soko huku akiwa hana washauri wazuri vinaweza kuwa matokeo ya yale anayofanya sasa


Nandy kashindwa kushika moja, anachanganya mambo matatu kwa wakati mmoja

Bongo fleva

Bongo movie

Gospel

Hivi vitu vitatu huwa kamwe havipikiki chungu kimoja hata siku moja...kila kimoja kina chemistry yake, ladha yake na mashabiki yake... Lazima ujitambulishe na kukubalika kwenye moja ya makundi hayo


Kuchanganya bongo fleva na bongo movie ni kujiua kisanii kwakuwa iko wazi kabisa kuwa sisi wabongo na haya mambo ya sinema za kisasa tumefeli big time..HATUWEZI.. Sisi tuko vizuri kwenye mziki walau kwasasa


Kuchanganya bongo fleva na gospel ni sawa na kuzipambanisha falme mbili zenye kutofautiana kwenye kila kitu....leo uombe nogesha kesho uimbe Mungu ni mwema ...HUTAELEWEKA KAMWE... Utajimaliza mwenyewe


Figa tatu alizochagua Nandy hazirandani asilani..anatawanya na kupoteza nguvu zake bila kujua.....Na hapaswi kutafuta mchawi kwenye hili zaidi ya washauri wake


Shetani akizeeka huwa malaika.. Usitake kuwa malaika kabla hujazeeka. Yuko wapi Stara Thomas? Mzee Yusuph ndio huyo anatanga na njia sasa...Kuna wakongwe kama Cosmas Chidumule na Mzee Makassy hawa walipoamua kuipa dunia kisogo na kumgeukia Mungu hawakuyumba wala kurudi nyuma.


Kina TID wameamua kuingia bongo movie kwakuwa hawana nafasi tena kwenye soko la mziki...huko wanalazimisha tuu...ili walau siku zisonge


Kwa umri wake Nandy na kipaji kilichomtoa cha bongo fleva angejenga mhimili imara kwanza huko.... Wakati anahangaika na bongo movie kina Zuchu wanampiku kwenye chart za umaarufu...!!!


All in all kama kaamua moja la kumrudia Mola wake na kuimba Gospel katika umri huo , awe na nia thabiti ya kiroho asije akageuka na kurudi alikotoka...ataishia kuchanganyikiwa... Kumrudia Mungu ni vita sio bata... Amuige Hafsa Kazinja...


Kama anashaurika basi atulie na kuanza upya na ashike moja tuu kwakuwa mshika mawili moja humponyoka...sasa yeye kashika matatu kwa mpigo...!!!Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz