"Mwanaume Mpe Pesa Mwanamke, sio Kuhonga" - Careen - EDUSPORTSTZ

Latest

"Mwanaume Mpe Pesa Mwanamke, sio Kuhonga" - Careen


Baby Mama wa msanii Barakah The Prince ambaye ni Video Vixen Careen Simba amesema ni jukumu la mwanaume kumpa pesa mpenzi wake na anavyompa sio kama ana muhonga bali ni kumlinda na kumudumia.


"Mwanaume kumpa pesa mwanamke ni jukumu lake kwa kweli na kama mwanamke wako lazima umuhudumie ingawa na yeye anatakiwa afanye kazi sio kila kitu mpaka amwambie mwanaume wake, ni jukumu la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke sio kama unamuhonga bali ni kumjali ili asije akaangaliwa na watu wengine mwisho wake akusaliti" ameeleza Careen Simba 


Kwa sasa mrembo huyo anaigiza filamu na ametokea kwenye video ya wimbo mpya wa Kala Jeremiah pia amefunguka chanzo cha kuachana na Barakah The Prince alikuwa ni Najdattan.

 No comments:

Post a Comment