Mwambusi Ashusha Presha ya Kocha Mpya Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwambusi Ashusha Presha ya Kocha Mpya Yanga-Michezoni leo

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa uamuzi wa kumpa timu kocha wao Juma Mwambusi mpaka mwishoni mwa msimu, umepunguza presha kubwa waliyokuwa nayo katika mchakato wa kumtangaza kocha mpya atakayekuja kufundisha kikosi hicho.

 

Yanga ipo kwenye mchakato wa kumtangaza kocha mpya atakayekuja kuchukua nafasi ya kocha Mrundi, Cedric Kaze aliyetimuliwa Machi 7, mwaka huu, ambapo Mfaransa, Sebastian Migne anatajwa kuwa kwenye nafasi kubwa ya kutwaa mikoba hiyo.

 

Mpaka Ligi Kuu Bara inasimama kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa, Yanga imesalia kuwa vinara wa msimamo ambapo wamecheza mechi 23 na kukusanya pointi 50.Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema:

 

“Uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na kamati yake ya ufundi unaendelea na mchakato wa kufanya upembuzi wa wasifu (CV), za makocha ambao waliwasilisha maombi ya kazi kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa kocha wetu Cedric Kaze.

 

“Tunatarajia kuweka wazi jina la kocha mkuu hivi karibuni, lakini kabla ya kufikia maamuzi ya kumpa timu kocha Mwambusi, kama uongozi tulikuwa na presha kubwa sana ya kusaka kocha mpya ili kuziba nafasi ya Kaze.

 

“Lakini kwa sasa mchakato huo hauna presha kubwa kwa kuwa tuna imani kubwa na kocha Mwambusi, na ndiyo maana tumekubaliana kumpa timu mpaka mwishoni mwa msimu.”

The post Mwambusi Ashusha Presha ya Kocha Mpya Yanga appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz