Mwambusi Akabidhiwa Mikoba ya Kaze-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwambusi Akabidhiwa Mikoba ya Kaze-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

IMEELEZWA kuwa baada ya Cedric Kaze raia wa Burundi kufutwa kazi ndani ya kikosi hicho mikoba yake atakabidhiwa mzawa Juma Mwambusi ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

 

Mwambusi alijiweka kando ndani ya Yanga kutokana na kile ambacho alieleza kwamba hakuwa kwenye afya bora na alishauriwa ajitenge na kazi ambazo zitahusisha kelele ama kuzungumza kwa muda mrefu.

 

 

Baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar akiwa na Kaze, Mwambusi aliomba kujiweka kando na Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla alithibitisha suala hilo.

 

 

Hivi karibuni Mwambusi alisema kuwa yupo fiti kiafya baada ya kurejea kwenye ubora wake jambo ambalo linatoa nafasi kwake kurejea kwenye majukumu ya kufundisha.

 

 

“Kwa sasa ninaendelea salama na nipo sawa hivyo ninaamini kwamba ninaweza kurejea kwenye majukumu yangu hali itakapokuwa sawa kwa asilimia 100,” alisema.

 

 

Kwa sasa Yanga haina benchi la ufundi baada ya Kaze kufutwa kazi Machi 7 baada ya ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kusoma 1-1 na kufanya timu hiyo kugawana pointi mojamoja na Polisi Tanzania.

 

 

Ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 50 kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo ilianza mzunguko wa kwanza ikiwa na Mwambusi pamoja na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ambaye naye alifutwa kazi. Kesho timu inatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi mzunguko wa pili.

The post Mwambusi Akabidhiwa Mikoba ya Kaze appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz