Man United Yaitungua Man City Mbili Kavu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Man United Yaitungua Man City Mbili Kavu-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa vijana wake walipambana kwa hali na mali na kufanikiwa kusepa na pointi tatu muhimu mbele ya Manchester City.

 

 

Baada ya dakika 90 kukamilika Uwanja wa City of Manchester ubao ulisoma, Manchester City 0-2 Manchester United ambapo mabao ya United yalipachikwa na Bruno Fernandes dakika ya pili kwa penalti na Luke Shaw dakika ya 50.

 

 

Ushindi huo unaifanya United kufikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya pili huku City ikibaki nafasi ya kwanza na pointi zake ni 65 na zote zimecheza jumla ya mechi 28.

 

 

 

Bruno amesema kuwa ni kazi kubwa kupiga penalti hasa unapopewa majukumu hayo kwenye presha ya kusaka ushindi jambo ambalo huwa linampa tabu.

 

 

“Ni ngumu kupiga penalti ndani ya ligi hasa pale unapoaminiwa na huwa inakuwa presha kubwa kwangu pamoja na timu kiujumla ila huwa tunafurahi pale ambapo tunashinda,” .

The post Man United Yaitungua Man City Mbili Kavu appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment