Lwandamina Ashtukia Mchongo Azam FC, Afanya Maamuzi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Lwandamina Ashtukia Mchongo Azam FC, Afanya Maamuzi-Michezoni leo

George Lwandamina.

KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina ameshtukia mchongo, hii ni baada ya kuahirisha mapumziko ya wiki mbili ya kikosi chake, na kuamuru nyota wote ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu ya taifa warudi kambini kujiandaa na maandalizi ya michezo yao ijayo.

 

Hapo awali Azam FC walipanga kuwa na mapumziko ya wiki mbili ili kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa, lakini wakaamua kubadili haraka mpango huo na kuwarudisha nyota wote ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa ili kuanza mazoezi.

 

Azam FC inakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi na pointi zao 44 walizokusanya baada ya kucheza michezo 24, huku wakizidiwa kwa pointi mbili tu dhidi ya Simba walio kwenye nafasi ya pili na pointi zao 46 baada ya kucheza michezo 20.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema:“Tofauti na mpango wetu wa mwanzo wa kuipa timu mapumziko ya wiki mbili kupisha ratiba ya michuano ya kimataifa, kuendana na mahitaji ya uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi lililo chini ya Kocha George Lwandamina tumefanya mabadiliko kidogo na tayari kikosi kimerejea kambini na kuanza mazoezi.

 

“Hii ni kwa sababu tunataka kuhakikisha wachezaji wetu wanakuwa na utimamu wa mwili wa kutosha ili kuweza kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo, kwa kukusanya pointi nyingi zaidi kwenye michezo yetu ijayo ambazo bila shaka zinaweza kutupa nafasi ya kushindania ubingwa.”

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam

The post Lwandamina Ashtukia Mchongo Azam FC, Afanya Maamuzi appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz