Kapo ya Mama Dangote Yazua Kasheshe! - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kapo ya Mama Dangote Yazua Kasheshe!


Ama kweli Waswahili hawana
jema! Hilo limethibitika usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya baadhi ya mashambenga waliohudhuria onesho la Cheka Tu kuisengenya kapo ya mama mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ na mpenzi wake, Anko Shamte.

Wawili hao waliibua minong’ono baada ya kuoneshana mahaba niue mbele ya umati uliofurika kwenye onesho hilo. Katika tukio hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, wawili hao waliingia ukumbini kama maharusi waliokuwa wakifurahia honeymoon na haikuwa rahisi kuamini kuwa penzi la wawili hao lina zaidi ya miaka mitano.

Wakati burudani ya Cheka Tu ikiendelea, wawili hao walizidi kuoneshana mahaba motomoto huku wakilishana ‘aisikrim’ za bei mbaya.

Mama Dangote na Anko Shamte walionekana kama vile wanamrusha roho mtu fulani kwani mara kadhaa waliinuka na kusindikizana maliwatoni.

Mama Dangote alipohitaji kwenda maliwatoni kurekebisha vazi lake kidogo, Anko Shamte alimsindikiza na kuishia mlangoni kumsubiri ‘kidekule wake’ na ilipofika zamu ya Anko Shamte, mambo yalikuwa tena hivyohivyo.

Wakati mahaba ya wawili hao yakizidi kuwa shatashata kupita kina, hali hiyo ilionekana kuwakera baadhi ya mashambenga wenye vijuso waliokuwa wanawafuatilia ambao walianza kuwasengenya.

Mmoja wa wasengenyaji hao alisikika akiguna na kusema eti penzi lao ni la moto wa mabua na haliwezi kufika popote, akisahau kwamba lina zaidi ya miaka mitano sasa. Msengenyaji huyo alisema penzi la wawili hao haliwezi kudumu na kutolea mfano wa mapenzi shatashata ya waliowahi kuoneshana baadhi ya wapenzi kisha kuangukia kifo cha mende.

“Unafikiri kuna mapenzi basi, ni usanii mtupu, hebu ona wanavyochezeana na kulishana, wapenzi watakuwa hawa bwana?

“Watu tumeona makeke ya Sarah na Harmonize, kapo ya Jux na Vanessa, Wema na Diamond, itakuwa wao? Ninyi subirini tu mtaniambia,” alisema shambenga huyo huku Mama Dangote na Anko Shamte wake wakiendelea kula raha za Dunia.

Stori; Richard Bukos, DarJe wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz