Jembe Jipya Larudisha Tabasamu Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Jembe Jipya Larudisha Tabasamu Yanga SC-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KUREJEA kwa jembe jipya la Yanga ndani ya kikosi hicho, unaweza kusema tabasamu la Wanayanga limerudi, hii ni baada ya timu yao kwa siku za karibuni kuonekana kuyumba kidogo.

 

Dickson Job ambaye ni beki mpya wa kati wa Yanga, alikuwa nje ya kikosi hicho kwa muda kidogo ambapo baada ya kupona majeraha yake, alipata matatizo ya kifamilia, lakini sasa ameyatatua na kurudi kambini.

 

Job ambaye hajaichezea Yanga mchezo wowote tangu atue kikosini hapo kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, kurejea kwake huenda kukaimarisha zaidi safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Akizungumza na Spoti Xtra,Job alisema: “Baada ya kumaliza changamoto za kifamilia ambazo zilinikumba hivi karibuni, natarajia kujiunga na kikosi kesho (jana) Jumamosi kwa ajili ya kujiandaa na michezo iliyo mbele yetu.

 

“Sijapata nafasi ya kuichezea Yanga mpaka sasa kutokana na changamoto mbalimbali, lakini naamini kwa kuwa kila kitu sasa kimekaa sawa, nitajitahidi kuhakikisha najituma kuisaidia timu yangu kila nitakapopata nafasi ya kucheza.”

STORI NA JOEL THOMAS | SPOTI XTRA

The post Jembe Jipya Larudisha Tabasamu Yanga SC appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment