Ibenge: Tunahitaji Pointi 3 Kwa Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ibenge: Tunahitaji Pointi 3 Kwa Simba-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa ili waweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanatakiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia ya ligi hiyo, dhidi Simba na Al Merrikh.

 

AS Vita kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika mara baada ya kujikusanyia pointi 4 nyuma ya Simba wenye 10 na Al Ahly wana saba.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Ibenge alisema kuwa kulingana na matokeo na pointi ambazo wamezipata wanatakiwa kushinda michezo yao miwili ijayo bila kujali wanakutana na timu ipi kwani wasipofanya hivyo hawatakuwa na uwezo wa kusonga mbele kuelekea katika hatua ya robo fainali.

 

“Tunatakiwa kushinda michezo yetu yote miwili iliyosalia dhidi ya Simba na Al Merrikh ili tuweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali, matokeo tuliyopata hayakuwa mazuri sana kwetu lakini huu si muda wa kulaumiana tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tunasonga mbele.

 

“Tunatakiwa kutojali tunacheza na mpinzani wa aina gani, michezo yote iliyosalia ni migumu kwetu tunacheza na Simba tukiwa ugenini mara ya mwisho tulipoteza mchezo pale hivyo hatutakiwa kurudia makosa, mchezo wa mwisho tutakuwa nyumbani kila mtu anafahamu hatujashinda hata mchezo mmoja kwetu pia tunatakiwa kurekebisha hili,” alisema kocha Ibenge.

 

AS Vita wanatarajia kucheza na Simba ugenini Aprili 2, katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar huku mchezo wa mwisho ukitarajiwa kufanyika DR Congo Aprili 9 dhidi ya Al Merrikh.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es salaam

The post Ibenge: Tunahitaji Pointi 3 Kwa Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz