Gomes Aliandaa Jembe Jipya la CAF Kumrithi Wawa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Aliandaa Jembe Jipya la CAF Kumrithi Wawa-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes ameanza kumuandaa beki wake mpya raia wa Zimbabwe, Peter Muduhwa katika kuelekea mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.Simba inatarajiwa kuvaana na Al Merrikh ya Sudan Jumanne ijayo saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Timu hizo katika mchezo wa awali uliopigwa Khartoum nchini Sudan, ulimalizika kwa suluhu kukiwa na ushindani mkubwa katika kila timu.

Katika mchezo huo wa marudiano, Simba itawakosa nyota wake wawili tegemeo, beki Pascal Wawa na Taddeo Lwanga wanaotumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Wakati akiwakosa wachezaji hao, kocha huyo ameonekana kuwaandaa baadhi ya wachezaji watakaochukua nafasi zao kati ya hao ni Muduhwa ambaye yeye juzi alimpa dakika 90 kucheza mchezo wa kirafiki waliocheza dhidi ya Dar City FC.

 

Katika mchezo huo uliopigwa saa kumi kamili jioni juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena uliopo Bunju, Dar Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na nahodha John Bocco.

 

Beki huyo katika mchezo huo alipangwa kucheza pamoja na mkongwe Erasto Nyoni katika safu ya ulinzi ya kati huku namba sita akicheza Said Ndemla.Gomes hivi karibuni alisema kuwa: “Nina imani na kila mchezaji wangu, hivyo ninao wachezaji wengi watakaokuwa mbadala wa Wawa na Lwanga.“Hivyo mara baada ya mchezo huu wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons haraka nitaanza maandalizi hayo ya kuwaandaa wachezaji hao ili kuhakikisha mapengo yao hayaonekani.”

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

The post Gomes Aliandaa Jembe Jipya la CAF Kumrithi Wawa appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz