Dube Majanga Tena, Nje Wiki Mbili Azam FC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Dube Majanga Tena, Nje Wiki Mbili Azam FC-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MAJANGA! Ndivyo utakavyoweza kusema kwa mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube ambaye anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili akiuguza maumivu ya misuli ya paja.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe arejee uwanjani akitokea katika majeraha ya bega yaliyomsababishia apelekwe Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Nyota huyo, hiyo itakuwa kwa mara ya pili mfululizo kukaa nje ya uwanja akiuguza majeraha tangu aliporejea uwajani wiki tatu zilizopita.

 

Kwa mujibu wa Daktari Mkuu wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa mshambuliaji huyo atakaa nje kwa kipindi kirefu kutokana na ukubwa wa majeraha hayo.

Mwankemwa alisema kuwa mshambuliaji huyo amepumzishwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu huku akifanya mazoezi mepesi ya binafsi kwa ajili ya kujiweka sawa.

 

“Ni kweli kabisa Dube atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili akiuguza maumivu ya misuli ya paja aliyoyapata katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mwadui FC.

Stori na Wilbert Molandi,Dar es Salaam

The post Dube Majanga Tena, Nje Wiki Mbili Azam FC appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment