Bale, Hazard Waongoza Kwa Mishahara Real Madrid-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bale, Hazard Waongoza Kwa Mishahara Real Madrid-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MISHAHARA ya Real Madrid imefichuka, huku ikionyesha kuwa wachezaji walioshindwa kukidhi matarajio ya mashabiki, Gareth Bale na Eden Hazard ndiyo wanakomba kitita kikubwa zaidi klabuni hapo.

 

 

Real Madrid ni timu ya soka ya pili duniani kwa kulipa mishahara mikubwa, ikiwa nyuma ya Barcelona pekee.Bale anaongoza akiwazidi wenzake mbali sana akipokea kitita cha pauni 650,000 (Sh bilioni 2) kila wiki, licha ya kuwa hayupo katika mipango ya kocha Zinedine Zidane na ameshapelekwa kwa mkopo Tottenham.

 

 

Tottenham ilikubali kuchangia nusu ya mshahara wa Bale ili kumnasa kwa mkopo, ikimaanisha kuwa inatoa paun 325,000 kila wiki huku Madrid nao wakitoa kiasi kama hicho.

 

 

Eden Hazard, anafuatia akiwa anachukua mshahara wa pauni 416,000 (Sh bil 1.3) kwa wiki.Mbelgiji huyo, 30, amecheza mechi 24 tu za La Liga tangu ajiunge akitokea Chelsea mwaka 2019 kwa donge nono la pauni milioni 88 ambalo linaweza kufikia hadi pauni mil 150.

 

 

Gwiji wa klabu hiyo, beki Sergio Ramos anachukua mshahara wa pauni 312,000 kwa wiki, wakati viungo Toni Kroos na Luka Modric wakipokea pauni 210,000 kila mmoja.

 

 

Wachezaji wengine 12 wa klabu hiyo wanapokea kitita cha pauni 100,000 au zaidi kila mmoja.Straika aliyefeli Luka Jovic ambaye sasa anacheza kwa mkopo Eintracht Frankfurt, anapokea pauni 175,000 kwa wiki huku Karim Benzema akipokea pauni 166,000.

 

 

Thibaut Courtois, Raphael Varane na Marcelo wanapokea pauni 150,000 kwa wiki kila mmoja.Dani Carvajal, Isco, Alvaro Odriozola, Lucas Vazquez, Marco Asensio, Eder Militao na Borja Mayoral ni wachezaji wengine wanaopokea kitita cha pauni 100,000 au zaidi kwa wiki.

 

 

Wanaopokea chini ya hapo ni Andriy Lunin (pauni 50,000), Ferland Mendy (pauni 53,000), Federico Valverde (pauni 62,000).

The post Bale, Hazard Waongoza Kwa Mishahara Real Madrid appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz